Wakuu wa mikoa wapewa rungu kuzuia machinga barabarani

September 2, 2026 4:01 pm · Shakrath Habibu
Share
Tweet
Copy Link
  • Awataka kuwarudisha machinga katika masoko waliyopangiwa, kutatua kero.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza wakuu wa mikoa kusimamia zoezi la kuwaondoa machinga barabarani na kushughulikia kero zinazolikabili kundi hilo.

Kauli ya Rais Samia inakuja ikiwa ni miezi sita tangu kuanza kwa utekelezaji wa marufuku ya machinga kutokupanga bidhaa zao barabarani iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila.

Licha ya maagizo ya mkuu huyo yaliyotolewa Machi 4 mwaka huu, utekelezaji wake umekuwa ukisuasua huku baadhi ya machinga wakiripotiwa kurudi barabarani hususani katika baadhi ya barabara za Kariakoo.

Akizungumza katika hafla ya uapisho wa viongozi wapya iliofanyika katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar leo Septemba 2, 2026, Rais Samia amewataka wakuu hao kutumia mbinu rafiki kuwarudisha machinga katika maeneo yao.

“Twende tukasimamie hayo si kwa kuwapiga fimbo na wale askari wa akiba sijui mgambo kwenda kuwanyanganya vitu vyao na kupiga mateke,hapana ni kwa mipango mizuri , tuwapangie mipango mizuri watoke waliko warudi kwenye masoko;” amesema Rais Samia.

Rais Samia Suluhu (Katikati) akiwa kwenye picha na wakuu wa mikoa baada ya hafla ya uapisho wa viongozi mbalimbali iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar tarehe 02 Septemba, 2026. Picha/ Ikulu Mawasiliano.

Dar, Dodoma, Mwanza na Arusha, Mbeya vinara

Aidha, Samia amebainisha kuwa tabia ya wafanyabiashara kurudi kufanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa inajurudia kwa kiasi kikubwa licha Serikali kujenga masoko makubwa katika majiji kama Dar es Salaam,Dodoma,Arusha, Mwanza pamoja na Mbeya.

Kiongozi huyo wa nchi amewataka wateule wake ngazi ya mkoa kushughulikia sababu za machinga hao kurudi barabarani ikiwemo kupanua masoko na kuanzisha njia mpya za daladala zinazofika katika masoko hayo.

“Na kama kelele ni daladala hazifiki kule hakuna  wateja tengeneza ruti daladala zishushe pale ili wafanyabiashara wapate wateja wa kununua bidhaa zao kuna mambo madogo madogo yanayowafanya watoke warudi  mitaani nendeni kasimamie lakini maeneo mengine ni ufinyu wa nafasi katika masoko mapya yaliyojengwa halmashauri jitahidini mjenge masoko mengine;” amesema Rais Samia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
2 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
2 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Majibu ya Serikali: Uhaba wa wataalamu wa ganzi, ajira 10,009 kutolewa

Majibu ya Serikali: Uhaba wa wataalamu wa ganzi, ajira 10,009 kutolewa

Nukta TV

Shangazi aibana Serikali kuhusu hadhi ya madereva, Prof. Kitila aingilia kati

Shangazi aibana Serikali kuhusu hadhi ya madereva, Prof. Kitila aingilia kati

Nukta TV

Haya ndio mambo ya kufanya bosi wako akikutongoza

Haya ndio mambo ya kufanya bosi wako akikutongoza

Nukta TV