Serikali yajipanga kukabiliana na mvua za El Niño

August 27, 2026 4:18 pm · Shakrath Habibu
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya ya TMA kutangaza ujio wa mvua kubwa za El Niño kuanzia Septemba hadi Januari, 2027.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali imeanza kujipanga kukabiliana na mvua za El Niño zinazotarajia kuanza mwezi ujao katika mikoa mbalimbali nchini.

Nchemba aliyekuwa akizungumza wakati wa maswali na majibu bungeni Dodoma  leo Agosti 27, 2026 amesema mbali na kutoa tahadhari Serikali imejipanga kurekebisha miundombinu ili kupunguza athari ya mvua hizo.

”Serikali imejipanga vyema kwa kuhakikisha maeneo yanayoweza kuwa na athari  za mvua nyingi kuandaa au kutengenezea mifereji ili maji yaweze kwenda kwenye njia zake ili kuondoa uwezekano wa maji kulundikana;” amesema Nchemba akijibu swali na Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini, Jonston Mtasingwa (CCM). 

Kauli hiyo ya Nchemba  imekuja ikiwa ni takribani  siku 11 tangu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Ladislaus Chang’a, atoe tahadhari ya uwepo wa  hali hiyo mbaya ya hewa itakayoambatana na mvua kubwa.

Chang’a, alisema kuwa ongezeko la mvua linatarajiwa zaidi Novemba 2026, huku mvua ambazo kwa kawaida huisha Desemba zikitarajiwa kuendelea hadi Januari 2027.

 Mvua za juu ya wastani hadi wastani zinatarajiwa hususani katika mikoa nane pamoja na maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria kwa mujibu wa TMA. Picha/BBC Swahili.

“Mvua hizo zinaweza kusababisha mafuriko, unyevu kupita kiasi kwenye udongo, uharibifu wa mazao na miundombinu, pamoja na kuongezeka kwa magonjwa ya mazao na milipuko kutokana na uchafuzi wa maji,” ilionya TMA.

Sambamba na onyo hilo, jana Agosti 26,2026, Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde aliwasihi wananchi kuweka akiba ya chakula walichovuna sasa ili kujihami na changamoto za kiuzalishaji zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.

Aidha Nchemba amewarai Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya mvua hizo akiwataka kufanya tathmini ya maeneo wanayoishi ikiwa yanaweza kuathirika na mvua hizo.

“  Naomba kuchukua nafasi hii kutoa  rai kwa watanzania wote kuwa na tahadhari na jambo hili tayari tumekwisha tahadharishwa ni wajibu wa  kila mtanzania pia kufanya tathmini ya aina hiyo pale anapoishi kwa kuangalia mazingira ya mahali na hali hii ambayo tumetahadharishwa,” ameongeza Nchemba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Dk Nchimbi afukuzwa CCM, Ndejembi akipendekezwa kuchukua mikoba

Dk Nchimbi afukuzwa CCM, Ndejembi akipendekezwa kuchukua mikoba

Nukta TV

Haya hapa mafao ya Dk Emmanuel Nchimbi aking’atuka madarakani

Haya hapa mafao ya Dk Emmanuel Nchimbi aking’atuka madarakani

Nukta TV

SIMULIZI: Namna Magufuli, Samia walivyoichonga historia ya Bwawa la Mwalimu Nyerere

SIMULIZI: Namna Magufuli, Samia walivyoichonga historia ya Bwawa la Mwalimu Nyerere

Nukta TV