Dola ya Marekani yaimarika kwa Sh5 NMB, CRDB
- Hii inamaanisha kuwa wanunuaji wa dola kupitia benki ya NMB watalazilima kutoboa mfuko zaidi kulinganisha na jana
Dar es Salaam. Dola ya Marekani imeendelea kuimarika dhidi ya Shilingi ya Tanzania, huku viwango vya leo vikionesha kuwa Benki za CRDB na NMB zimefikia viwango sawa vya ubadilishaji wa Dola.
Kwa mujibu wa viwango vya ubadilishaji fedha vilivyotolewa leo Julai 30, 2026, Dola ya Marekani inanunuliwa kwa Sh2,605 na kuuzwa kwa Sh2,685 katika benki zote mbili, CRDB na NMB.
Hii ni tofauti na Jana Julai 29,2026 ambapo Benki ya CRDB ilinunua Dola kwa Sh2,600 na kuuza kwa Sh2,680, huku NMB ikiwa na viwango vya juu zaidi vya Sh2,605 kwa ununuzi na Sh2,685 kwa uuzaji.
Hii inamaa kuwa upande wa CRDB, Dola imeongezeka kwa Sh5 kwenye bei ya kununua na Sh5 kwenye bei ya kuuza ndani ya siku moja. Wakati huo huo, NMB imeendelea na viwango vyake vya jana bila mabadiliko, hali iliyosababisha benki zote mbili kuwa na viwango vinavyofanana leo.
Kwa wafanyabiashara na watu binafsi wanaohitaji kununua Dola kwa ajili ya malipo ya bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi, ongezeko hilo linamaanisha watahitaji kutumia Shilingi zaidi kwa kila Dola wanayonunua ukilinganisha na siku zilizopita.
