Dola ya Marekani yaongezeka kwa Sh5 NMB

July 10, 2026 9:36 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • NMB leo inanunua dola kwa Sh2,595 na kuiuza kwa Sh2,675, kutoka Sh2,590 na Sh2,670 zilizotumika jana Julai 9. 

Dar es Salaam. Benki ya NMB imeongeza viwango vya kununua na kuuza Dola ya Marekani kwa Sh5 leo Julai 10, 2026, hali inayoashiria shinikizo la kuongezeka kwa gharama za fedha za kigeni katika soko la ndani.

Uchambuzi wa viwango vya kubadilisha fedha uliofanywa na Nukta Habari unaonyesha kuwa NMB leo inanunua dola kwa Sh2,595 na kuiuza kwa Sh2,675, kutoka Sh2,590 na Sh2,670 zilizotumika jana Julai 9. 

Hii inamanisha kuwa wafanyabiashara watakaonunua Dola ya Marekani katika benki ya NMB watalazimika kutumia gharama kubwa zaidi kwa kila dola moja kulinganisha na jana.

Kwa upande wa Benki ya CRDB, viwango vya kubadilisha fedha hiyo vimebakia bila mabadiliko, ambapo bei ya kununua imesalia kuwa Sh2,590 na kuuuzwa kwa Sh2,670, sawa na viwango vya jana.

Mbali na Dola ya Marekani, sarafu za Ulaya zimeonyesha kupanda zaidi katika soko la leo. Katika benki ya CRDB, Euro imeongezeka kutoka kiwango cha ununuzi cha Sh2,844.7 jana hadi Sh2,852 leo, huku bei ya kuuza ikipanda kutoka Sh3,144.7 hadi Sh3,152.

Pauni ya Uingereza nayo imepanda katika benki zote mbili. Katika benki ya CRDB, Pauni imeongezeka kutoka Sh3,356 kwa ununuzi na Sh3,656 kwa uuzaji jana hadi Sh3,367.8 na Sh3,667.8 leo. NMB pia imepandisha viwango vyake vya pauni kutoka Sh3,321 kwa ununuzi na Sh3,666 kwa uuzaji jana hadi Sh3,341 na Sh3,686 leo.

Kwa upande wa sarafu za kikanda, Shilingi ya Kenya na Uganda zimeendelea kuwa tulivu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
10 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
10 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
10 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
130 wakamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuhamasisha uhalifu Tanzania

130 wakamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuhamasisha uhalifu Tanzania

Nukta TV

Mfumuko wa bei Tanzania wapungua kwa 0.2%

Mfumuko wa bei Tanzania wapungua kwa 0.2%

Nukta TV

Rais Samia awaonya wanaharakati wenye matendo ya kigaidi

Rais Samia awaonya wanaharakati wenye matendo ya kigaidi

Nukta TV