Mikoa 5 iliyoongoza kwa makosa ya usalama barabarani 2025

May 22, 2026 9:53 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Licha ya kuwa ya kuwa mkoa ulioongoza kwa matukio, ilala imerekodi vifo vya watu 12, vifo vichache zaidi kuliganisha mikoa mingine.

Dar es Salaam. Makosa ya usalama wa barabarani yameendelea kuongezeka nchini Tanzania licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Polisi.

Takwimu za hali ya uhalifu na matukio ya usalama barabarani zinaonesha makosa hayo yameongezeka kwa asilimia 2.3  kutoka makosa 3,104,501 mwaka 2024  hadi makosa 3,174,724  kufikia Desemba 2025.

Hata hivyo, pamoja na ongezeko hilo la kitaifa, baadhi ya mikoa ya kipolisi imeendelea kurekodi idadi kubwa ya makosa ya usalama barabarani yaliyochangia kutokea kwa ajali, vifo pamoja na majeruhi kwa watumiaji wa barabara. 

Leo Nukta TV tunakuletea mikoa 5 ya kipolisi iliyoongoza kwa makosa ya barabarani Tanzania bara.

Mkoa wa tano ni Morogoro uliorekodi makosa177,902 yaliyo sababisha vifo vya watu 70 wake kwa waume. 

Licha ya Morogoro kushika namba tano kimatukio, ni mkoa wa pili ambao umesababisha idadi kubwa ya vifo vitokanavyo na ajali.

Mkoa wa 4 ni mkoa wa Pwani ambao kwa mwaka 2025 umerekodi makosa 189,477 yaliyosababisha vifo vya watu 28. 

Mkoa wa kipolisi wa Temeke umeshika nafasi ya 3 ukirekodi makosa 215,154 kwa mwaka 2025, huku makosa haya ya usalama barabarani katika mkoa huo yakisababisha vifo vya watu 33.

Mkoa wa 2 ulioongoza kwa makosa ya usalama barabarani 2025 ni mkoa wa Kinondoni uliorekodi makosa 300,514 yaliyoondoa maisha ya watu 102 wake kwa waume. 

Licha ya mkoa huu kushika nafasi ya pili, ndio mkoa ulioongooza kwa idadi kubwa ya vifo katika orodha hii.

Kwa mwaka 2025 mkoa wa kipolisi wa Ilala ndio mkoa ulioongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya matukio ya usalama barabarani ukirekodi matukio 356,340 mara mbili zaidi ya mkoa wa Morogoro, 

Licha ya kuwa ya kuwa mkoa ulioongoza kwa matukio, ilala imerekodi vifo vya watu 12, vifo vichache zaidi kuliganisha mikoa mingine.

Kwa mujibu wa takwimu za hali ya uhalifu matukio haya yamesababishwa na sababu mbalimbali ambapo asilimia 96.2 ni makosa ya kibinadamu ikiwemo uzembe wa madereva, asilimia 2.2 ubovu wa vyombo vya usafiri na asilimia 1.6 ubovu wa miundombinu na mazingira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

/
No matches found for this filter
22 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
23 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
23 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

Nukta TV