Dola yaimarika kwa Sh5 CRDB, Sh8 NMB, Mei 21, 2026

May 21, 2026 9:03 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa siku ya tatu mfululizo sarafu hiyo inazidi kuimarika katika benki hizi mbili za kibiashara nchini.

Dar es Salaam. Dola ya Marekani yaendelea kuimarika dhidi ya Shilingi ya Tanzania kwa siku ya tatu mfululizo ikiongezeka kwa Sh5 katika benki ya CRDB na Sh8 NMB kwa bei ya kuuza na kununua.

Kwa mujibu wa takwimu za viwango vya kubadilisha fedha vya leo Mei 21, 2026, Dola ya Marekani katika benki ya CRDB inauzwa kwa Sh2,660 na kununuliwa kwa Sh2,580.

Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 0.19 kulinganisha na Sh2,655 kwa bei ya kuuza na Sh2,575 kwa bei ya kununua zilizotumika hapo jana.

Hali kama hiyo imeonekana NMB ambapo leo Dola ya Marekani imeongezeka kwa Sh8 hadi kuuzwa kwa Sh2,663 kutoka Sh2,655 ya jana huku bei ya kununua ikipanda hadi Sh2,583 kutoka Sh2,575.

Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 0.3 kwa bei ya kuuza na kununua katika benki ya NMB ukilinganisha na viwango vilivyotumika jana Mei 20, 2026.

Hii inaonyesha kuwa wafanyabiashara na waagizaji bidhaa watakaotumia dola kupitia benki ya NMB watalazimika kutumia kiasi kikubwa zaidi cha fedha kulinganisha na jana, huku gharama zikiendelea kuwa nafuu kidogo kwa wanaobadilisha fedha kupitia CRDB.

Katika sarafu nyingine, Euro imeonyesha kushuka kidogo katika benki ya CRDB ambapo bei ya kununua imeshuka kutoka Sh2,883.8 hadi Sh2,877.51 na kuuza kushuka kutoka Sh3,183.8 hadi Sh3,177.51.

Kwa upande wa Sterling ya Uingereza, Shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika kidogo katika CRDB huku pauni ikiuzwa kwa Sh3,648.87 kutoka Sh3,652.2 ya jana.

Aidha, sarafu za kikanda ikiwemo Shilingi ya Kenya, Rand ya Afrika Kusini na Yuan ya China zimeendelea kubaki katika mabadiliko madogo, hali inayoashiria utulivu wa soko la fedha za kigeni nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

/
No matches found for this filter
22 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
23 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
23 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

Nukta TV