Dola ya Marekani yaongezeka kwa Sh5 CRDB
- Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 0.19 kwa siku ya pili mfululizo kwa benki ya CRDB ukilinganisha na Sh2,655 kwa bei ya kuuza na Sh2,575 kununua iliyotumika jana Mei 19, 2026.
Dar es Salaam. Dola ya Marekani imeendelea kuimarika dhidi ya Shilingi ya Tanzania ikiongezeka kwa Sh5 katika benki ya CRDB ikibaki tulivu NMB.
Kwa mujibu wa takwimu za viwango vya kubadilisha fedha leo Mei 20, 2026, Dola ya Marekani inauzwa kwa Sh2,680 na kununuliwa kwa Sh2,660 katika benki ya kibiashara ya CRDB.
Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 0.19 kwa siku ya pili mfululizo kwa benki ya CRDB kulinganisha na Sh2,655 kwa bei ya kuuza na Sh2,575 kununua iliyotumika jana Mei 19, 2026.
Hata hivyo hali imeonekana tofauti katika benki ya NMB ambapo Dola ya Marekani imeendele kusalia katika kiwango sawa na jana ikiuzwa kwa Sh2,655 na kununuliwa kwa Sh2,575.

Ongezeko hilo ni sawa asilimia 0.19 kwa bei ya kuuza na kununua ukilinganisha na bei iliyotumika jana Mei 18, 2026 ambapo dola iliuzwa kwa Sh2,650 na kununuliwa kwa 2,570.
Hii inamaanisha kuwa kwa wafanyabiashara watakao badili fedha zao katika benki ya CRDB gharama itaongezeka kwa Sh5 zaidi kulinganisha na watakao badili kupitia benki ya NMB.
Hivyo kwa upande wao itawalazimu kutoboa mifuko yao zaidi kufanya uagizaji wa bidhaa kutoka nje kama mafuta na bidhaa nyingine muhimu.
Hata hivyo, hali imeonekana tofauti kwenye sarafu nyingine kama Euro na sarafu za kikanda ikiwemo Shilingi ya Kenya na Uganda ambapo Shilingi ya Tanzania imeendelea kuwa tulivu.
Latest