Tume: Watu 518 walipoteza maisha vurugu Uchaguzi Mkuu 2025

April 23, 2026 4:57 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tume uliofanywa kwa siku 153.
  • Rais Samia aahidi matibabu bure na vifaa saidizi kwa wahanga.

Arusha. Watu 518 wakiwemo watoto wadogo walipoteza maisha wakati wa vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 2025 huku zaidi ya watu 2,000 wakijeruhiwa. 

Mwenyekiti wa tume ya rais iliyoundwa kuchunguza matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Mohamed Chande Othman amesema vifo hivyo vya Watanzania si vya kawaida (Unnatural deaths).

Katika hotuba yake wakati akiwasilisha ripoti ya uchunguzi wa matukio hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan leo Aprili 23, 2026 jijini Dar es Salaam, Chande amesema kati ya watu waliofariki dunia wakati wa matukio hayo, 490 walikuwa wanaume, 28 wanawake na watoto 21.

Kati ya maiti 518 zilizobainishwa na ripoti ya tume hiyo, maiti 480 sawa na asilimia 92.7 zilitambuliwa na kuchukuliwa na familia zao.

Mwenyekiti huyo amesema kati ya watu waliofariki dunia, 373 walifikishwa hospitali wakiwa wamefariki na majeruhi 121 walifariki wakati wanapata matibabu hospitali na maiti 24 bado hazina taarifa kamili.

Pamoja na waliopoteza maisha Chande, ambaye aliwahi kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, amesema kufikia Machi, 2026 watu 2,390 walijeruhiwa kwenye vurugu hizo huku asilimia 95 wakiwa raia na asilimia tano ni maofisa wa Jeshi la Polisi.

Takwimu hizo za idadi ya vifo zinajibu maswali ya muda mrefu ya Watanzania waliotaka kujua idadi kamili ya waliopoteza maisha katika ghasia hizo zilizo acha alama katika maisha ya Watanzania wengi.

Miongoni mwa waliofariki ni watoto 21 na maskari wa vyombo vya ulinzi na usalama 16. 

Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria hafla ya kuwasilisha ripoti ya uchnguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani ya Oktoba 29, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 23, 2026.

Hata hivyo, Chande amesema huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi kuzikwa na ndugu zao bila kufikishwa kwenye vituo vya afya au baadhi ya ndugu kutofika mbele ya tume. 

Chande amesema pia kuna uwezekano wa baadhi ya watu kufariki wakati wakijiguza majeraha nje ya mfumo rasmi na taarifa zao kutofikishwa sehemu husika. 

“Idadi ya vifo hivyo 518 vya ripoti ya tume inaweza ikawa sio kauli ya mwisho yaani ‘final and conclusion’,” amesema Chande.

Tume hiyo inawasilisha ripoti hiyo leo ikiwa ni siku 153 tangu kuundwa kwake na Rais Samia Novemba 18, 2025 ikilenga kuchunguza na kubainisha sababu na madhara yaliyojitokeza katika vurugu hizo.

Rais Samia Suluhu aliyekuwa akizungumza baada ya kupokea ripoti hiyo amesema kuwa vifo hivyo vimeacha maumivu makubwa katika mioyo ya Watanzania wengi.

“Kivyovyote vile walioumizwa na tukio lile ni sisi Watanzania, ni sisi tuliopoteza watoto wetu, ni sisi tuliopoteza ndugu zetu jamaa na marafiki zetu, kwa hali yoyote ile walioathirika ni Watanzania kwa ujumla wetu haiwezekani mtu mwingine asiye Mtanzania awe na uchungu zaidi kuliko sisi Watanzania, haiwezekani,” amese Rais Samia.

Ili kutibu mioyo hiyo iliyoachwa na majeraha Rais Samia amesema Serikali yake itaandaa utaratibu maalum wa kugharamia matibabu kwa Watanzania ambao bado wana majeraha pamoja na kutoa vifaa saidizi kwa baadhi ya wahanga wa vurugu hizo.

Chadema yapinga ripoti ya Jaji Chande

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeipinga vikali ripoti hiyo kikisitiza kuwa mchakato wake ulikuwa batili.

“Chadema inasitiza kuwa ripoti hii na mchakato wake wote ni batili…haiwezekani mtuhumiwa akajichunguza mwenyewe halafu tutarajie haki,”imesema taarifa ya Brenda Rupia, Mkurugenzi wa mawasiliano na uenezi wa chama hicho.

Aidha, Chadema imesema inaendelea kufanya uchambuzi wa muhutasari wa ripoti uliosomwa na Jaji Mohamed Chande Othman pamoja na hotuba iliyotolewa baada ya kupokelewa kwa ripoti hiyo. Kauli kamili ya Chama itatolewa baada ya kikao cha Kamati Kuu kitakachofanyika tarehe 28 na 29 Aprili 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: WABUNGE WAKIJADILI HOTUBA YA WIZARA YA NISHATI BUNGENI

🔴LIVE: WABUNGE WAKIJADILI HOTUBA YA WIZARA YA NISHATI BUNGENI

Nukta TV

🔴LIVE: NDEJEMBI AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI WIZARA YA NISHATI

🔴LIVE: NDEJEMBI AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI WIZARA YA NISHATI

Nukta TV

🔴LIVE: RAIS SAMIA, MAMALISHE,  BABALISHE WANAJAMBO LAO LEO

🔴LIVE: RAIS SAMIA, MAMALISHE, BABALISHE WANAJAMBO LAO LEO

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.