Sekta 5 zilizoongoza kwa faida, uwekezaji wa kigeni (FI) Tanzania 2024

Kwa mujibu wa ripoti ya uwekezaji ya mwaka 2025, faida halisi (net profit baada ya kodi) inayopatikana kutokana na uwekezaji wa kigeni (FI) iliongezeka hadi kufikia Sh5.78 trilioni mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 20.67 kutoka Sh4.79 trilioni mwaka 2023.
Faida nyingi zilitokana na sekta kuu kama fedha na bima, ambayo iliongoza kwa takribani Sh2.26 trilioni, ikifuatiwa na uchimbaji madini na mawe Sh1.72 trilioni, pamoja na sekta ya viwanda Sh0.78 trilioni.
Hata hivyo, mgao wa faida (dividends) uliotangazwa ulipungua kwa asilimia 27.7 hadi kufikia Sh1.31 trilioni, kutokana na mabadiliko ya kimkakati ambapo wawekezaji walichagua zaidi kubakiza faida zao ndani ya biashara badala ya kuzigawa.
Kwa upande mwingine, uwekezaji upya wa faida (reinvestment of earnings) uliongezeka kwa kiasi kikubwa hadi kufikia Sh4.47 trilioni.
Latest