ATCL inavyopoteza mabilioni kila mwaka

March 31, 2026 9:51 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link

Licha ya Februari 6, 2026, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa kusema kuwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) linaendelea kuimarika likionesha ukuaji chanya na kukusanya jumla ya mapato ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 157 (sawa Sh404.5 bilioni) tangu kuimarishwa kwake upya.

Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini kuwa ATCL ilipata hasara ya Sh191.19 bilioni katika mwaka wa fedha 2024/25 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa gharama za uendeshaji.

CAG Charles Kichere aliyekuwa akiwasilisha ripoti ya ukaguzi wake Machi 30, 2026 mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan amesema hasara hiyo imeongezeka kwa asilimia 108 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja ikiongezeka maradufu tangu kuanzishwa kwake.

“ATCL imefikisha jumla ya hasara ya Sh 748 bilioni tangu kuanzishwa kwake licha ya kuendelea kupata ruzuku za Serikali kwa ajili ya mishahara na gharama za uendeshaji,” amesema CAG Kichere.

Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa ATCL kutajwa kuwa miongoni mwa mashirika ya umma yanayotengeza hasara nchini.

Mwaka 2022/23 ATCL lilitengeneza hasara ya Sh56.6 bilioni iliyoongezeka kutoka Sh35.2 bilioni mwaka 2021/22 kabla ya kupaa tena mwaka 2023/24 kufikia 91.7 bilioni licha ya uwekezaji unaoendelea kufanywa na Serikali katika shirika hilo.

Kwa mujibu wa Kichere, hasara hiyo imechangiwa na mambo mbalimbali ikiwemo ongezeko la gharama za uendeshaji kuzidi ukuaji wa mapato ambapo gharama ziliongezeka kwa Sh 134 bilioni na kufikia Sh675 bilioni.

Aidha, amesema matumizi yasiyo bora ya ndege ya mizigo aina ya Boeing 767-300F yamechangia hasara hiyo, ambapo asilimia 90.4 ya safari zilikuwa za masafa mafupi na ya kati badala ya safari ndefu zenye mapato makubwa.

Kutokana na Hali hiyo ndege ilisimamishwa huku ikiendelea kugharimu shirika takribani Sh bilioni 3.5 kwa ukodishaji na bima bila kuzalisha mapato.

Pia CAG ameeleza kuwa udhaifu wa mifumo ya udhibiti umepelekea malipo ya Sh20.61 bilioni kwa mawakala bila kuthibitishwa kuwafikia abiria, pamoja na marejesho ya fedha kwa abiria ya Sh 31.7milioni yaliyofanyika bila nyaraka za kuthibitisha uhalali wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.