Rais Samia awataka viongozi wateule kuwajibika

February 9, 2026 4:05 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema wasiokwenda na kasi ya serikali watapisha wengine.
  • Ataka utekelezaji wa majukumu uendane na mahitaji ya wananchi.

Dar es Salaam.Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi waliokula kiapo cha uadilifu katika nafasi mbalimbali Serikalini kufanya kazi kwa uwajibikaji, uadilifu na kasi ili kukidhi matarajio ya wananchi.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza leo  Februari 9, 2026, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uapisho wa viongozi hao a mabadiliko yaliyofanyika ni sehemu ya hatua za kuharakisha maendeleo ya taifa na kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya serikali.

“Mabadiliko haya ni katika jitihada za kuendana na kasi ya utekelezaji, lengo ni kuenda na kasi ya matarajio au mahitaji ya wananchi,” amesema Samia.

Aidha, Rais Samia ameweka wazi kuwa jicho lake litakuwa kwa kila mteule kufuatilia utendaji wao wa kazi, akibainisha kuwa mfumo wake wa uongozi unahitaji watu wenye utayari wa kubadilika na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi.

“Ukiona hatua zako haziendani na ngoma ninayoipiga, utatupisha wengine wenye miguu myepesi waendelee,” amesisitiza Rais Samia

Mbali na uwajibikaji wa jumla, Rais amewataka viongozi hao kufungua milango kwa sekta binafsi na kuondoa ukiritimba wa kisheria unaokwamisha uwekezaji. 

Ameeleza kuwa lengo la Serikali ni kuona sekta binafsi inachukua sehemu kubwa ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ili kukuza uchumi wa taifa.

Pia, amejibu maoni ya watu wanaohusisha mabadiliko ya viongozi na migogoro, akifafanua kuwa anafanya hivyo ili kukuza vipaji na kuwapa viongozi uzoefu katika sekta tofauti.

“Kazi yangu ni kulea na kukuza, si kulea na kudumaza. Na ndio maana wengi niliowalea nawatoa nawapa posti nendeni kafanyeni, nasukuma vipaji mbele,” amefafanua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks