Viwango vya kubadili fedha Februari 9, 2026

February 9, 2026 9:39 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link

Viwango vya kubadilisha fedha za kigeni dhidi ya Shilingi ya Tanzania vinavyotolewa na Benki za CRDB na NMB kwa matumizi ya leo Februari 9, 2026. Dola ya Marekani imeendelea kusalia katika kiwango sawa na kilichokuwa wiki iliyopita cha Sh2,568 kwa bei ya kununua na Sh2,648 bei ya kuuza kwa benki zote mbili.

Viwango hivi hubadilika kila siku kulingana na mwenendo wa soko la fedha, na vina umuhimu mkubwa kwa wafanyabiashara, wawekezaji na walipakodi, hasa katika kufanya malipo ya ada, kodi pamoja na ununuzi na uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Kupitia viwango hivi vya kubadilisha fedha, watumiaji wa sarafu za kigeni hupata mwongozo sahihi wa kupanga bajeti, kufanya manunuzi na kuendesha shughuli zao za kifedha kwa ufanisi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks