Rais Samia afanya uteuzi PSSF, Tanesco

December 12, 2025 10:32 am · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  •  Fortunatus Makore Magambo na Plasduce Mkeli Mbossa ndio viongozi walioteuliwa.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wapya katika taasisi mbili za umma ili kuboresha utendaji kazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba 11, 2025  na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu, akirejea taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka, Fortunatus Magambo ni miongoni mwa walioteuliwa.

“ Fortunatus Makore Magambo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Magambo alikuwa Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi katika mfuko huo nafasi aliyoitumikia tangu mwaka 2018.

Uteuzi wa Magambo, unaziba nafasi iliyoachwa wazi na Dk Rhimo Nyansaho ambaye Novemba 10, 2025, aliteuliwa kuwa mbunge na baadaye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Dk Nyansaho alihudumu katika mfuko huo kuanzia Mei 26, 2025 alipoteuliwa kwa mara ya kwanza, akitokea Benki ya Azania kwa nafasi ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara.

Rais Samia pia amemteua Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mkeli Mbossa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Mbossa anaenda kurithi mikoba ya Dk Nyansaho ambaye ndiye aliyekuwa ameishikiria nafasi hiyo hadi uteuzi huu ulipofanyika akiwa ameiongoza bodi hiyo kuanzia Desemba mwaka 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks