Serikali yasisitiza uwekezaji unaogusa maisha ya vijana

November 28, 2025 5:40 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Yatoa wito kwa wawekezaji kuelekeza miradi yao katika sekta zenye uwezo wa kukuza uchumi na kuongeza mauzo nje ya nchi.

Dar es Salaam. Serikali imesisitiza kuwa mwelekeo mpya wa uwekezaji nchini unatakiwa kulenga kutatua changamoto za kiuchumi zinazowakabili Watanzania hasa vijana, kwa kuwafungulia fursa za ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof Kitila Mkumbo aliyekuwa akizungumza leo Novemba 28, 2025 jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi na Watoa Huduma wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (Tiseza), amesema Serikali inataka aina ya uwekezaji unaojibu mahitaji halisi ya wananchi.

“Nataka niwapeni maelekezo maalumu yanayolenga kuwapa mikakati itakayochochea uwekezaji unaojibu shida za kiuchumi za Watanzania, hususan fursa za ajira kwa vijana,” amesema Prof. Mkumbo.

Prof Mkumbo, ameeleza kuwa katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji, wahusika wanapaswa kuhakikisha shughuli zote za uwekezaji zinaendana na vipaumbele vilivyobainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ikiwemo kuimarisha ajira, kuongeza uzalishaji, na kukuza uchumi shindani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo katika picha ya pamoja na viongozi wa Tiseza. Picha/ Goodluck Gustaph/Nukta habari

Aidha, Prof Mkumbo ameeleza umuhimu wa uwekezaji unaoonekana katika maisha ya wananchi wa kawaida, akionya dhidi ya uwekezaji wa kwenye televisheni ambao hauonyeshi matokeo kwa wananchi.

“Uwekezaji usiojibu shida za Watanzania hauwezi kutusaidia. Tunataka uwekezaji ambao vijana wakisoma takwimu wajione humo, mama lishe ajione humo, boda boda ajione humo. Hatuwezi kuzungumzia uwekezaji wakati wananchi bado hawana ajira,” amesema Prof Mkumbo.

Tiseza ni muunganiko wa Taasisi ya Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) ilioanzishwa mwaka huu lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Kupitia bodi mpya, Prof Mkumbo amesema Serikali ina imani kuwa taasisi hiyo itaboresha uratibu wa shughuli za uwekezaji na kuongeza ushindani wa Tanzania katika kuvutia wawekezaji.

Prof Mkumbo amefafanua kuwa bodi ya Tiseza imepewa jukumu la kuhakikisha vigezo hivyo vinatumika katika kupendekeza maeneo ya uwekezaji na vivutio vinavyostahili kutolewa kwa wawekezaji.

Sanjari na hayo pia amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imebainisha vigezo vitano muhimu vya kuchagua sekta za kimageuzi ambavyo bodi inapaswa kuzingatia, vikiwemo uwezo wa sekta kuzalisha ajira nyingi hasa kwa vijana na  uwezo wa kuongeza mauzo ya bidhaa nje ya nchi (export potential).

Vile vile, nafasi ya sekta kuchochea ukuaji wa sekta nyingine, uwezo wa kuongeza thamani ya bidhaa (value addition), na mchango wa sekta katika kuongeza mapato ya Serikali.

Hata hivyo, Prof Mkumbo ameongeza kuwa serikali itaendelea kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji, akitoa wito kwa Tiseza kushirikiana kwa karibu na Serikali na wadau wa sekta binafsi ili kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa kivutio kikubwa cha uwekezaji barani Afrika.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
11 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
12 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
12 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Akili Unde (AI) ni suluhu ya habari za uzushi ?

Akili Unde (AI) ni suluhu ya habari za uzushi ?

Nukta TV

KAOMBWE: Mfungwa aliyegeuza gereza kuwa darasa la ujuzi Mwanza

KAOMBWE: Mfungwa aliyegeuza gereza kuwa darasa la ujuzi Mwanza

Nukta TV

BoT yafungua soko la dhamana za Serikali kwa wawekezaji wa kigeni

BoT yafungua soko la dhamana za Serikali kwa wawekezaji wa kigeni

Nukta TV