Zungu achaguliwa kuwa Spika mpya Tanzania

November 11, 2025 1:16 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baaada ya kupata kupigiwa kura na wabunge kwa asilimia 98.6.

Arusha. Aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mussa Azzan Zungu kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Tanzania baada ya kupata kura 378 kati ya kura 383 zilizopigwa.

Zungu ambaye ni mbunge  wa jimbo la Ilala amewamwaga wagombea wengine waliokuwa wanawania nafasi hiyo kwa kupata asilimia 98.6 ya kura zote zilizopigwa.

Zungu alikuwa akichuana na wagombea wengine akiwemo Veronica Charles Tyeah kutoka Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA),

Anitha Alfan Mgaya kutoka Chama cha National League for Democracy (NLD) na Chrisant Nyakitita kutoka Chama cha Democratic Party (DP).

Wengine ni Ndonge Said Ndonge kutoka Chama cha Alliance for Africa Farms Party (AAFP) na Amin Alfred Yango kutoka Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).

Uchaguzi huo umefanyika leo Novemba 11, 2025 jijini Dodoma na kuongozwa na Mwenyekiti wa uchaguzi, Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi ambaye amepitishwa na wabunge kuongoza uchaguzi huo.

Kwa ushindi huo, Zungu anachukua nafasi ya Dk Tulia Ackson aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitatu tangu mwaka 2022 baada ya aliyekuwa Spika wa Bunge wa wakati huo Job Agustino Ndugai kujiuzuru Januari 6, 2022.

Aahidi ushirikiano kwa wabunge, Serikali

Baada ya kutangazwa mshindi Zungu amewashukuru wabunge kwa muchagua huku akihidi kutoa ushirikiano kwa wabunge hao pamoja na Serikali kwa ajili ya ustawi wa Tanzania.

“Niwahakikishie kuwa ushindi huu ni wetu sote, hamjanichagua ili niongoze Bunge lakini mmenichagua niwatumikie na kuhakikisha yale yote tuliyokubaliana kama vipaumbele vya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo yanafanikiwa…

…Naahidi kutoa ushirikiano kwa Serikali kwamba kama Bunge tuntashauri na kutoa maazimio ya Bunge kwa ajili ya ustawi wa wananchi na maendeleo endelevu kwa ustawi wa nchi yetu,” amesema Zungu.

Pamoja na hayo, Zungu amemshukuru mtangulizi wake Dk Tulia Ackson kwa kumpa mafunzo na maelekezo yaliyomjenga na kumuimarisha akiahidi kuyaendeleza kwa wasaidizi wake watakaochaguliwa akiwemo Naibu Spika.

“Ninaaahidi viongozi watakao chaguliwa kuwa wasaidizi wangu, Naibu Spika na baadae Wenyekiti wa Bunge,  tutashirikiana kuongoza Bunge hili la 13 kwa kutoa maamuzi ya haki na kuzingatia uadilifu…

…Hakutakuwa na upendeleo wowote tutaongoza kwa kufuata katiba sheria za nchi na kanuni za Bunge kwa vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni,” ameongeza Zungu.

Zungu ambaye amekuwa mbunge kwa miaka 20 anakuwa Spika wa nane atakayeliongoza Bunge hilo la 13 kwa miaka mitano ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks