Maoni mchanganyiko Watanzania wakijiandaa kupiga kura Oktoba 29
Dar es salaam. Zikiwa zimebakia siku mbili Uchaguzi Mkuu kufanyika, Watanzania wamekuwa na maoni tofauti kuhusu uchaguzi huo huku baadhi wakisema watatumia vizuri haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Uchaguzi Mkuu utafanyika Jumatano Oktoba 29, 2025 ambapo Watanzania watamchagua Rais, Wabunge na Madiwani.
Nukta TV imepita mitaani katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam, Mwanza na Arusha kuzungumza na Watanzania ili maoni ya jinsi walivyojiandaa na uchaguzi huo.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Nukta TV wapo ambao ni kwa mara ya kwanza wanashiriki Uchaguzi Mkuu na wengine wameshiriki chaguzi zilizopita.
Wamekuwa na maoni tofauti kulingana na maono yao pamoja na uzoefu wao katika ushiriki katika chaguzi zilizopita.
Zaidi tazama video hii
Latest