HESLB yatangaza majina waliopata mikopo awamu ya kwanza 2025/26

October 24, 2025 3:09 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • 40,952 ni wa shahada ya kwanza na 5,342 wa stashahada ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya Sh152 bilioni.

Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa awamu ya kwanza ya upangaji mikopo na ruzuku kwa jumla ya wanafunzi 135,240 nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, leo Ijumaa, Oktoba 24, 2025, kati ya wanafunzi hao, 40,952 ni wa shahada ya kwanza na 5,342 wa stashahada ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya Sh152 bilioni.

Aidha, wanafunzi 615 waliopo chini ya mpango wa Samia Scholarship wamepangiwa ruzuku yenye jumla ya Sh3.3 bilioni.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa wanafunzi 88,331 wanaoendelea na masomo wamepangiwa mikopo yenye thamani ya Sh271.2 bilioni baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka uliopita.

Bodi hiyo imebainisha kuwa itaendelea kutoa awamu nyingine za mikopo na ruzuku kadiri itakavyopokea uthibitisho wa udahili kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na matokeo ya wanafunzi wanaoendelea.

HESLB pia imewakumbusha waombaji wa mikopo na ruzuku kuendelea kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia mfumo wa Student’s Individual Permanent Account (SIPA) wakati taratibu za uchambuzi na upangaji zikiendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks