Chakwera akubali kushindwa katika uchaguzi mkuu Malawi

September 24, 2025 7:00 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Awataka wananchi kukubali ushindi huo na kuheshimu katiba ya nchi hiyo.

Arusha. Aliyekuwa Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera amekubali kushindwa na mpinzani wake Peter Mutharika katika uchaguzi wa Urais uliofanyika Septemba 16, 2025 kabla ya kutangazwa rasmi kwa matokeo ya uchaguzi huo.

Chakwera aliyekuwa akihutubia kwa njia ya televisheni  leo Septemba 24, 2025 amepongeza utendaji kazi wa tume ya uchaguzi huku akibainisha kuwa uamuzi wake ni sehemu ya kuheshimu katiba ya nchi hiyo. 

“Matokeo haya ni ishara utashi wenu wa kubadili Serikali kwa hivyo kitu sahihi pekee ni mimi kukubali matokeo kwa kukubali utashi wenu kama wananchi pamoja na kuiheshimu Katiba ya nchi yetu,” amesema Chakwera.

Kulingana na takwimu za awali, Peter Mutharika alipata zaidi ya asilimia 60  ya kura, ikilinganishwa na asilimia 24 za Chakwera.

Mutharika akitangazwa kuwa mshindi ataliongoza Taifa hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo baada ya kuwekwa kando katika uchaguzi wa mwaka 2020 akitarajiwa kupambana na umasikini uliokithiri pamoja mfumuko wa bei.

Peter Mutharika akizungumza na Wananchi katika moja ya kampeni zake nchini Malawi.Picha/ Malawi24.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia (WB), Malawi ni miongoni mwa nchi nne zenye viwango vya juu zaidi vya umasikini duniani, ambapo asilimia 70 ya watu wake wanaishi chini ya dola 2 kwa siku.

Utafiti wa kaya uliofanyika nchini humo mwaka 2019 ulibaini Idadi ya watu maskini imefikia milioni 13 ambapo nusu ya  idadi hiyo (asilimia 51) bado hawawezi kupata mlo wao wa siku.

IItakumbukwa kuwa Mutharika aliwahi kuliongoza Taifa hilo kwa awamu moja kuanzia mwaka 2014 hadi 2020 akiahidi kupunguza mfumuko wa bei uliokuwa umekithiri.

Mpaka kufikia mwaka 2020 utawala wake ulikabiliwa na kashfa za ufisadi na kushindwa kupunguza umaskini ambao ndiyo kilio kikubwa kwa Wamalawi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV