Arusha yaweka mikakati kuboresha miundombinu kuelekea AFCON 2027

September 23, 2025 4:45 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali yaahidi kuboresha barabara,na vifaa vya usalama, njia bora za usafirishaji wa mashabiki na timu.

Arusha. Jiji la Arusha limejipanga kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara ili kuvutia wageni watakaokuja katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2027 katika nchi za Tanzania , Kenya na Uganda  yanatajwa kuwa miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii nchini.

Kutokana na umuhimu wa mashindano hayo Serikali ilianza maboresho ya viwanja vya michezo vilivyopo pamoja na ujenzi wa uwanja mpya wa michezo jijini Arusha ambao ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 60.

Mbali na ujenzi wa uwanja huo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude amesema wanatarajia kukarabati miundombinu mbalimbali ya jiji hilo ikiwemo barabara kwa ajili ya kuvutia wageni.

“ Tayari mkakati na mchoro upo mipango miji kuhakikisha barabara zinapitika kuelekea viwanja vya michezo…

…Tumeshaanza mikakati ya kuwa na mabango na matangazo ya AFCON maeneo yote ya jiji lakini pia kuwa na nembo na kaulimbiu ya  Arusha kwa AFCON,” amesema Mkude aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo Septemba 23, 2025.

Kwa mujibu wa Mkude miundombinu mingine itakayoongezwa ni pamoja na vifaa vya usalama, njia bora za usafirishaji wa mashabiki na timu,taa za barabarani, bendera, sanaa ya mitaani na mapambo ya kiutamaduni.

Huenda ukarabati na maboresho hayo yanayotarajiwa kufanyika katika jiji hilo hususan maeneo ya pembezoni ambayo yanakabiliwa na ubovu wa miundombinu kwa kiwango kikubwa ukaongeza mvuto wa jiji hilo la kitalii.

Pamoja na miundombinu hiyo Mkude amesema watadhibiti takataka zinazozagaa hovyo mitaani kwa kuanzisha utaratibu wa kuzirejereza huku akiahidi uboreshaji wa masoko na vituo vya daladala ambavyo vyote vitaenda kuboresha jiji la Arusha.

Aidha, Mkude amesema watawachukulia hatua wale wote wanaohujumu miundombinu ya barabara na mwananchi atakayefanikisha kukamatwa kwa wahujumu hao wa miundombinu atazawadiwa Sh500,000.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
28 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
28 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
28 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Jinsi afya ya akili inavyowatesa wanawake makazini

Nukta TV

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV