Mbinu za kuthibitisha habari bila intaneti

September 3, 2025 11:23 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kusikiliza matangazo na habari kutoka mamlaka husika.

Arusha. Kuna namna nyingi za kuthibitisha habari zinazoweza kukusaidia kubaini ukweli hususani wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani unaotarajia kufanyika Octoba 29 mwaka huu.

Miongoni mwa namna hizo zipo ambazo hazihitaji matumizi ya intaneti zinazoweza kufanywa na wananchi wa kawaida wasiokuwa na simu janja au kompyuta ikiwemo kusikiliza matangazo na habari kutoka mamlaka husika.

Mbinu nyingine ni  kuwahoji wataalamu au mashuhuda kupata taarifa za uhakika hasa zinazohusu uchaguzi, kusoma nyaraka au takwimu za mamlaka rasmi za Serikali au taasisi binafsi.

Pamoja na hizo, unaweza kusoma magazeti na majarida yenye vyanzo vya uhakika vya taarifa. Pamoja na hibitisha kwa kwenda eneo husika na kufanya uchunguzi wa moja kwa moja.

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks