Slivery Luboja Ambwaga Mnyeti Kura za Maoni Misungwi

August 5, 2025 4:16 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Apata kura  3,249 kati ya zaidi ya 15,000 zilizopigwa na wajumbe 

Mwanza. Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Misungwi na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti, amekiri kushindwa katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) za kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo hilo, akieleza kuwa sasa atajielekeza kwenye shughuli nyingine za kujipatia kipato.

Mnyeti, ambaye alichaguliwa mwaka 2020 baada ya kumshinda aliyekuwa mbunge wa wakati huo, Charles Kitwanga, alipata kura 3,249 kati ya kura zaidi ya 15,000 zilizopigwa na wajumbe wa jimbo hilo. 

Katika uongozi wake, aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, nafasi anayoshikilia hadi sasa.

“Matokeo ndiyo hayo na mimi nimeyapokea kwa mikono miwili. Nilimshinda mtu na mimi nimeshindwa na mtu, na ndiyo utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi; tunashindana kwa kura na mwenye kura nyingi ndiye mshindi. Nawashukuru wananchi kwa kunipa miaka mitano,” amesema Mnyeti.

Amesema kazi siyo ubunge pekee, kwani zipo fursa nyingi nyingine zikiwemo kilimo, uvuvi na biashara, ambazo atajihusisha nazo baada ya kumaliza kipindi chake cha ubunge.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi, Emmanuel Masangwa, mshindi wa kura za maoni ni Slivery Luboja aliyepata kura 9,684, akifuatiwa na Mnyeti (3,249). 

Washindani wengine walikuwa John Kilangi (258), William Kafiti (202), Deusdediti Komanya (136) na Isa Lufungulo (85).

“Tunashukuru uchaguzi umekuwa huru na haki. Sasa jukumu limebaki kwa Kamati ya Maadili ya chama ambayo itatangaza mgombea halali atakayewakilisha CCM katika uchaguzi ujao,” amesema Masangwa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV