Luhaga Mpina ahamia ACT – Wazalendo baada ya kuachwa uteuzi wabunge CCM
- Ametambulishwa kwenye kurasa rasmi za chama hicho akiwa.
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa na Waziri wa zamani wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amehamia rasmi chama cha ACT Wazalendo leo Agosti 5, 2025.
Mpina ametambulishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya ACT Wazalendo akiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Dorothy Temu.
Uamuzi wa Mpina umekuja siku chache tu tangu jina lake lilipoachwa miongoni mwa walioteuliwa kuwania nafasi za ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).Â
Itakumbukwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia wakazi wa Mkoa wa Simiyu Juni 17, aliwaambia wakazi wa maeneo hayo kuwa Luhaga anafaa kuwa mbunge wa kitaifa kwa kuwa ameshindwa kuzisemea vyema changamoto za wakazi wa jimbo lake, na badala yake kujitafutia umaarufu.
Hata hivyo, Mpiana hajaweka wazi iwapo atagombea Ubunge katika jimbo la Kisesa au Urais kupitia chama hicho.Â
Iwapo chama hicho kitampa Mpina dhamana ya kugombea nafasi ya urais kitapaswa kutengua uamuzi wa awali uliotangazwa ambapo walimteua mwenyekiti wa chama hicho Dorothy Temu kuwa mgombea.
Mpina atakuwa si mwana CCMÂ wa kwanza kujiunga na upinzani baada ya kukosa fursa ya kugombea nafasi ya uongozi kwenye chama chake. Mwaka 2020 aliyekuwa kada wa muda mrefu wa CCM na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Benard Membe alihamia katika chama hicho baada ya kufukuzwa CCM ambapo alitaka kugombea Urais.
Membe hakushinda urais kupitia ACT Wazalendo na alirejea CCM mwaka 2021 ambapo mpaka umauti unamkuta alikuwa mwanachama wa CCM.
Mwaka 2015, Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa kada wa alihamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya jina lake kutopendekezwa kuwania urais kupitia CCM.
Licha ya Lowassa kuhamia Chadema na kusababisha ushindani mkali katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2025, hakufanikiwa kushinda nafasi ya urais na baadaye alirejea CCM.
Latest