Necta yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2024 ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 3

January 23, 2025 11:31 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link

Arusha. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika Novemba, 2024, ambapo ufaulu umeongezeka kiduchu.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Said Mohamed aliyekuwa akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo Januari 23, 2025 amesema kuwa  ufaulu umeongezeka kwa asilimia tatu kulinganisha na ufaulu wa mwaka 2023.

“Takwimu zinaonesha kuwa ufaulu wa jumla umepanda kwa asilimia tatu na hivyo kufikia asilimia 92.37 ambapo watahiniwa 477,262 kati ya watahiniwa  516,695 wenye matokeo wamefaulu kwa kupata daraja  la kwanza, la pili, la tatu na la nne,” amesema Dk Said.

Mwaka 2023 jumla ya watahiniwa 471,427 sawa na asilimia 89.36 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha nne waliofaulu mtihani huo.

Kwa mujibu wa Necta, jumla ya watahiniwa wa shule 529,329 walisajiliwa kufanya mtihani huo ambapo asilimia 98 sawa na watahiniwa 517,460 walijitokeza kufanya mitihani hiyo Novemba 11 hadi 29 mwaka 2024.

Watahiniwa 11,869 sawa na asilimia mbili hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali licha ya kuwa walisajiliwa.

Ubora wa ufaulu waongezeka

Dk Said amewaambia wanahabari kuwa ubora wa ufaulu kwa mwaka 2024 umeongezeka kwa asilimia 5.6 kulinganisha na ule wa mwaka 2023.

Ubora wa ufaulu hupimwa kwa kuangalia idadi ya wanafunzi waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ambapo kwa mwaka 2024 watahiniwa 221,953 sawa na asilimia 43 walipata madaraja hayo.

Mwaka 2023 waliopata ufaulu wa daraja ya kwanza hadi daraja la tatu walikuwa 197,426 sawa na asilimia 37.4.

Kwa mujibu wa Necta katika kipengele cha ubora wa ufaulu wavulana wamefanya vizuri zaidi kulinganisha wasichana.

“…Wavulana ni 119,869  sawa na asilimia 54 na wasichana 102,084 sawa na asilimia 46 hivyo Wasichana wamefaulu wengi zaidi wakati wavulana wamefaulu vizuri zaidi,”amesema Dk Said.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV