Necta yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2025 ufaulu waongezeka kwa asilimia 2.61

January 31, 2026 11:30 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link

Arusha. Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika Novemba, 2025, ambapo ufaulu umeongezeka kiduchu.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Said Mohamed aliyekuwa akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo Januari 31, 2026 amesema kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.61 kulinganisha na ufaulu wa mwaka 2024.

“Takwimu zinaonesha kuwa ufaulu wa jumla umepanda kwa asilimia 2.61 na hivyo kufikia asilimia 94.98 ambapo watahiniwa 526,620 wamefaulu kwa kupata dvision I, II, III, na IV, mwaka 2024 watahiniwa waliofaulu walikuwa 477,262 sawa na asilimia 92.37 na mwaka 2023 walikuwa 471,427 sawa na asilimia 89.36 ,” amesema Dk Said.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks