Viwango vya kubadili fedha za kigeni dhidi ya shilingi ya Tanzania leo Disemba 11, 2024
Dar es Salaam. Thamani ya shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika dhidi ya Dola ya Marekani iliyokuwa ikinunuliwa kwa Sh2,500.61 na kuuzwa Sh2,525.62 hadi kufikia jana Disemba 10, 2024. Jumatano ya leo Disemba 11 thamani ya dola kununuliwa imepungua kwa Sh82.11 na kuuzwa Sh2,418.5 huku ya kuuza ikipungua kwa Sh83.02 ikitoa ahueni kwa wafanyabiashara wanaotumia dola.
Pia wafanyabiashara wanaouza na kuagiza bidhaa China wana unafuu baada ya thamani ya Shilingi ya Tanzania kuendelea kuimarika dhidi ya sarafu ya China (CYN) kwa Sh10.73 kwa bei iliyokua ikinunuliwa jana sambamba na bei ya kuuzwa kwa Sh10.77.
Thamani ya shilingi imeimarika pia dhidi ya Euro kwa Sh100 kwa bei ya kununua sambamba na Sh101 kwenye bei ya kuuzwa kutoka jana iliponunuliwa kwa Sh2,647 na kuuzwa Sh2,674.
Bei ya dhahabu imeendelea kushuka mfulizo ndani ya wiki hii ambapo kutoka jana imepungua kwa Tsh98,558 na sasa inanunuluwa kwa Tsh6,475,280. Kwa upande wa uuzwaji bei imepungua kwa Tsh99,594.