Viwango vya kubadili fedha za kigeni dhidi ya shilingi ya Tanzania leo Disemba 10, 2024

December 10, 2024 9:39 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Thamani ya shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika dhidi ya Dola ya Marekani iliyokuwa ikinunuliwa kwa Tsh2,569.79 na kuuzwa Tsh2,595.49 hadi kufikia Ijumaa Disemba 6, 2024. Hadi kufikia Jumatatu ya leo wafanyabiashara wanaotumia dola kufanya malipo ya bidhaa wana ahueni ya Tsh69.18 huku bei ya kununua ikishuka kwa Tsh69.87.

Pia thamani ya Shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika dhidi ya sarafu ya China (CYN) kwa Tsh9.62 kwa bei iliyokua ikinunuliwa kutoka Tsh353.75. Bei ya kuuzwa nayo imepungua kwa Tsh9.72 kutoka Tsh357.19, kupungua huku kunatoa ahueni kwa wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka China.

Bei ya dhahabu kununuliwa imeshuka kwa Tsh240,710 kutoka Tsh6,814,548 iliyotumiwa Ijumaa na leo inauzwa 6,573,838 kwa mujibu wa viwango wa Benki kuu ya Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Enable Notifications OK No thanks