Serikali yazindua maboresho ya Sera ya maendeleo ya vijana kutatua changamoto zao

August 12, 2024 7:52 pm · Bacley Madyane
Share
Tweet
Copy Link
  • Maboresho yafanyika baada ya kupita miaka 17 tangu ilipoandikwa sera hiyo.
  • Miongoni mwa changamoto itakazotatua ni pamoja na kuanzishwa kwa baraza la vijana na kurasimisha shughuli za uzalishaji mali.

Dar es salaam. Huenda vijana wakapata mwamko mpya na kushiriki kikamilifu katika shughuli zinazochochea maendeleo kwa nchi ikiwemo za kisiasa, kiuchumi na kijamii mara baada ya Serikali kuzindua Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007 maboresho ya mwaka 2024.

Kwa muda mrefu vijana nchini Tanzania wamekuwa wakiitaka Serikali kufanya maboresho ya sera hiyo iliyoandikwa zaidi ya muongo mmoja uliopita kwa kuwa kwa haiakisi changamoto za sasa.

Ridhiwani Kikwete, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu aliyekuwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kimataifa yaliyofanyika leo Agosti 12, 2024 amewaambia washiriki kuwa maboresho ya sera hiyo yanakwenda kumaliza vilio vya vijana.

“Changamoto nyingi zinazoelezwa katika vijana zinatokana na ukweli kwamba, yako baadhi ya maeneo hayana miongozo yake, kupitia sera hii tunayoizindua leo nina uhakika kabisa vilio vya vijana walio wengi vinakwenda kupatia ufumbuzi baada ya kupitishwa kwa sera hii,” amesema Kikwete.

Kwa mujibu wa Kikwete miongoni mwa changamoto itayotatuliwa na sera hiyo ni kuanzishwa kwa baraza la taifa la vijana ambalo linatarajiwa kuwa mwarobaini wa changamoto zinazowakabili vijana.

“Vijana wamekosa maeneo ya kueleza changamoto zao, vijana walikosa watu wa kuwasikiliza, vijana walikosa mfumo wa kuwasilisha changamoto zao na kuzitafutia majawabu kwa pamoja, ujio wa sera hii ya vijana na uundwaji wa baraza hili la vijana ni dhahiri kuwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuhakikisha changamoto zote zinatafutiwa majawabu,” amebainisha Kikwete.

Itakumbukwa Rais Samia alipokuwa akizungumza na vijana wa Mkoa wa Mwanza  kwa niaba ya vijana wa Tanzania Juni 2021 aliahidi kuwa Serikali yake itakwenda kuangalia nini kilichosababisha kukwama kwa mchakato wa kuanzishwa kwa baraza la vijana jambo lililoombwa kwa muda mrefu. 

Kikwete ameongeza kuwa sera hiyo mpya inaenda kuwatambua vijana katika nyanja zote za uzalishaji mali ikiwemo wanaofanya kazi katika mazingira magumu.

Aidha, Kikwete amewataka maafisa kazi kutimiza wajibu wao kwa kutosubiri changamoto za vijana maofisini kwao, bali kuwatembelea katika maeneo yao, kubaini na kuzitatua changamoto walizonazo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo.

Vijana ndio kundi kubwa zaidi nchini Tanzania kwa sasa ambapo kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 asilimia 34.4 ya watu ni vijana ambao ni nguvu kazi ya Tanzania kwa asilimia 55.6%.

Miongoni mwa changamoto zinazolikabili kundi hilo ni pamoja na ukosefu wa ajira, kutotambulika rasmi kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi pamoja na kukosa fursa za kisiasa ambazo sera mpya inatarajiwa kuleta ufumbuzi wake.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
23 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Baba Levo: Wazo la kuongeza tozo kwenye bodaboda litolewe, tuleteeni watu wa tungi

Baba Levo: Wazo la kuongeza tozo kwenye bodaboda litolewe, tuleteeni watu wa tungi

Nukta TV

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV