Mtumbwi waua shabiki wa Yanga, watano hawajulikani

August 6, 2024 5:42 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link

Mwanza. Mtu mmoja amefariki dunia huku wengine watano wakiwa hawajulikani walipo baada ya mtumbwi waliokuwa wanasafiria kuingia maji na kuzama ndani ya Ziwa Victoria usiku wa kuamkia leo wakitoka kusherehekea wiki ya Mwananchi. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema hadi mtumbwi huo unazama uilikuwa na watu 23 ambao ni mashabiki wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga ambao walikuwa wanatoka kusherehekea kilele cha Wiki ya Mwananchi wilayani Sengerema.

Mutafungwa amewaambia wanahabari jijini Mwanza kuwa watu wengine 17 waliokuwepo kwenye mtumbwi huo walinusurika na ajali hiyo. 

“Watu hao walikuwa wanasafiri kutoka kisiwa cha Yozu kuelekea kisiwa cha Bulyaheke wilayani Sengerema ndipo mtumbwi huo ulipoanza kuingia maji na kusababisha kuzama,” amesema Mutafungwa. 

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV