Serikali kuinoa timu ya Taifa kuelekea michuano ya AFCON 2027

April 30, 2024 10:18 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Lengo ni kuhakikisha timu inafanya vizuri katika michuano hiyo.
  • Serikali yasema itawarejesha wachezaji wazawa waliopo nje ya nchi pamoja nakuajiri kocha na benchi la ufundi lenye sifa.

Dar es salaam. Huenda timu ya Taifa ya Tanzania ikafanya vizuri katika ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inayotarajiwa kufanyika mwaka 2027 mara baada ya Serikali kuanisha mikakati ya kuinoa timu hiyo.

AFCON ni michuano ya mpira wa miguu inayohusisha timu zilizopo barani Afrika ambapo Septemba 27, 2023 nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zilitangazwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.

Michuano hiyo mikubwa barani Afrika inarejea katika ukanda wa Afrika Mashariki baada ya miaka 47 tangu ifanyike nchini Ethiopia mwaka 1976.

Naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma, ameanisha mipango mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuwatumia wachezaji wazawa wanaocheza na kuishi nchi nje ya Tanzania. 

“Mkakati mwingine ni kuwatafuta na kuwaleta nchini wachezaji wenye asili ya Tanzania wanaoishi na kucheza nje ya nchi ili kuchezea timu ya Taifa…

…kuhakikisha timu ya Taifa inashiriki mechi za kirafiki na mataifa mbalimbali na kufanya kambi katika mazingira mazuri ili kuwa na maandalizi bora,” amesema Mwinjuma akijibu swali wa Mbunge wa Magomeni Mwanahamisi Said leo Aprili 30, 2024 Bungeni Dodoma.


Soma zaidi:Tanzania, Kenya Uganda wenyeji Afcon 2027


Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo itaendeleza ujenzi wa viwanja vya mpira jijini Dodoma na Arusha ili kutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya maandalizi ya timu ya Taifa.

Serikali imepanga  kuwashirikisha wadau wa michezo kuchangia timu za Taifa kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali fedha za kugharimia timu za Taifa zinazoshiriki mashindano ya kimataifa.

Katika hatua nyingine, Serikali imesema itashirikisha wadau wa michezo kuchangia timu za Taifa kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali fedha pamoja na kuajiri kocha na benchi la ufundi lenye sifa na uzoefu katika mpira wa miguu duniani.

Serikali pia imeandaa mpango maalum utakao washindanisha wasanii kutunga nyimbo kwa ajili ya michuano hiyo zitakazotumika kama sehemu ya burudani ambapo wimbo utakaoshinda ndio utakaotumika.

Enable Notifications OK No thanks