TASAC:Tumeanza kuchunguza chanzo cha meli kuzama ziwa Victoria

May 21, 2024 10:22 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Uchunguzi huo utashirikisha wataalamu wabobezi wa masuala ya miundombinu ya meli, mitambo na mifumo ya uundaji wa meli.

Mwanza. Shirika la Uwakala wa meli Tanzania (TASAC) limeanza kufanya uchunguzi wa chanzo cha kupinduka na kuzama kwa Meli ya MV. Clarias ikiwa ni siku mbili tangu kutokea kwa tukio hilo jijini Mwanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAC, Mohamed Salum aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza baada ya kutembelea eneo la tukio leo Mei 21, 2024 amesema ili kukamilisha uchunguzi huo watazungumza na  wafanyakazi wa meli ikiwemo nahodha na mabaharia.


Soma zaidi:Kimbunga IALY kusababisha mvua, upepo kwa siku mbili Tanzania


“Baada ya kutembelea eneo la tukio tumeanza uchunguzi wa kitaalamu kubaini kilichosababisha meli kulalia upande mmoja kabla ya kuzama majini ikiwa imetia nanga Bandari ya Mwanza Kaskazini…

…Tutazungumza na wafanyakazi (nahodha na mabaharia) kufahamu meli ilikuwa na changamoto gani watusaidie kabla ya uchunguzi utakaohusisha chombo chenyewe,” amesema Salum.

Uchunguzi wa meli hiyo iliyojengwa mwaka 1961 utashirikisha wataalamu wabobezi wa masuala ya miundombinu ya meli, mitambo na mifumo ya uundaji wa meli.

Mwonekano wa meli ya Mv. Claries ikiwa inaonekana nusu mgongo baada ya kupinduka na kuzama ndani ya Ziwa. Picha na Mariam John/ Nukta

Juhudi za kuitoa meli ziwani zinaendelea

Salum amebainisha kuwa tangu kutokea kwa tukio hilo Mei 19, 2024 juhudi za kuitoa majini meli hiyo ya MV.Clarias zinaendelea ambapo Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) ikishirikiana na kampuni ya Songoro Marine na Mkombozi Transport zinashirikiana kuitoa meli hiyo.

“Sababu za kiufundi meli kuzama ni mashaka ya kufikirika, yawezekana ilikunywa maji (yaliiingia) ikiwa imetia nanga ikalalia upande mmoja,kwa nini iliingiza maji hicho ndicho tunachokitafuta,”amesema Salum.

Baada ya zoezi hilo kukamilika meli hiyo itapelekwa kwenye chelezo Mwanza Kusini kwa uchunguzi na watakachobaini kisha wataishauri Serikali hatua za kuchukua.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV