Dar es Salaam kinara kwa idadi kubwa ya migogoro ya ardhi Tanzania

May 28, 2024 7:15 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Migogoro yafikia 4,486 sawa na asilimia 38 ya migogoro yote nchini.
  • Mikoa mingine iliyoongoza ni Dodoma, Mwanza,Tabora na Tanga.

Dar es Salaam. Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa idadi kubwa ya migogoro ya ardhi nchini Tanzania jambo linalotishia ustawi wa shughuli za kiuchumi na kijamii zinazohitaji rasilimali hiyo.

Kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 migogoro ya ardhi iliyopokelewa katika mkoa huo kwa ni 4,486.

Migogoro ni ile iliyopokelewa katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 15, 2024.

Idadi ya migogoro iliyopo mkoani Dar es Salaam ni asilimia 38 ya migogoro yote 11, 860 iliyopo nchini.

Hotuba hiyo inabainisha kuwa kati ya migogoro 3285 kati ya iliyoripotiwa jijini Dar es salaam imetatuliwa sawa na asilimia 73.2 imetatuliwa na kupatiwa ufumbuzi.

Mbali na Dar es Salaam mikoa mingine iliyoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya migogoro ni pamoja Dodoma yenye jumla ya migogoro 2,331 na jiji la Mwanza lenye migogoro 1,181

Mingine ni  mkoa wa Tabora ulioripoti migogoro 627 na Tanga migogoro 512.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV