Kesi ya Kabendera yaahirishwa kwa saa 24

February 10, 2020 9:05 am · Nuzulack Dausen
Share
Tweet
Copy Link
  • Imeahirishwa hadi kesho Februari 11, 2020 kutokana na kutokamilika upelelezi. 
  • Hii ni mara ya kwanza kesi hii inaahirishwa na kupangiwa terehe ya karibu zaidi kwa siku moja pekee.

Dar es Salaam. Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera imeahirishwa hadi kesho kutokana na kutokamilika upelelezi. 

Mashtaka yanayomkabili mwanahabari huyo anayeandikia  vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi ni kuongoza kundi la uhalifu kwa lengo la kupata faida au manufaa mengine, kutokulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya zaidi ya Sh173.24 milioni na utakatishaji wa fedha kiasi cha  zaidi ya Sh173.24 milioni.

Wakili wa Serikali, Faraji Nguka ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo (Februari 10, 2020) kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo anaomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa.

Kesi hiyo iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega ilifikishwa mahakamani leo kwa ajili ya kutajwa.

“Uchunguzi wa kesi hii unaendelea na ikikupendeza Mheshimiwa Hakimu uipangie tarehe nyingine ya kesho,” amesema Nguka.


Soma zaidi: 


Wakili kiongozi wa Kabendera, Jebra Kambole ameiambia mahakama kuwa hawana na kipingamizi juu ya maombi hayo ya wakili wa Serikali.

Mtega ameiahirisha kesi hadi kesho.

Hii ni mara ya kwanza kesi hii inaahirishwa na kupangiwa terehe ya karibu zaidi kwa siku moja pekee.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV