Fahamu ‘kisima’ cha taarifa za chanjo za corona duniani

June 16, 2021 1:14 pm · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Unaweza kujua ni chanjo ngapi zimetengezwa na ngapi zimeruhusiwa.
  • Kupitia mfumo huu utaweza kujua kila hatua ya chanjo iliyokuwa katika majaribio.

Dar es Salaam.Tangu chanjo ya ugonjwa wa virusi vya corona (Covid-19) ipatikane kumekuwa na sintofahamu kubwa inayosababisha kusambaa kwa taarifa nyingi za uzushi dhidi ya chanjo hiyo muhimu katika maisha ya binadamu. Hali hiyo imefanya  mashirika, kampuni na taasisi mbalimbali ulimwenguni kuja na mikakati ya kukabiliana na habari hizo.

Miongoni mwa mashirika hayo ni Shirika la Habari la Marekani la New York Times liliounda mfumo wa kidigitali  ujulikanao kama “Coronavirus Vaccine Tracker” ukiwa ni mfumo wenye taarifa lukuki kuhusu chanjo za corona.

Mfumo huo unaeleza mambo mbalimbali ikiwemo idadi ya chanjo zilizotengezwa na zile zilizofanyiwa majaribio.

Pia mfumo huo wa unaeleza ni chanjo gani zimeruhusiwa kutumiwa na zimetengenezwa na kutoka nchi gani na taasisi gani huku zikiwa na maelezo ya ziada ya kitabibu kuhusu utumiaji wake.

Miongoni mwa taarifa hizo ni idadi ya mtu kufikia kiwango kamili cha chanjo inayotakiwa kumkinga kikamilifu dhidi ya maradhi hayo yanayozidi kuutesa ulimwengu.

‘Coronavirus Vaccine Tracker’ ni moja ya mifumo mizuri inayosaidia kutoa elimu ya chanjo kwa kiasi kikubwa ulimwenguni hivyo pale unapokutana na taarifa unayoitilia mashaka huna budi kutembelea katika mfumo huu na kuweza kujiridhisha uhakika wa taarifa hizo .

Hadi sasa Shirika la Afya Duniani (WHO) limeruhusu chanjo za Astra Zeneca/Oxford vaccine, Johnson and Johnson, Moderna,  Pfizer/BionTech, Sinopharm na  Sinovac kutumika ulimwenguni ili kuwakinga watu na maradhi ya Covid-19.

Miongoni mwa chanjo hizi zinatumiwa na baadhi ya mataifa ya jumuiya ya Afrika Mashariki kama Kenya, Uganda na Rwanda ambazo zimeanza kuwachanja raia wake.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW