Lupin II: Filamu inayoelezea mwanzo wa uhalifu wa kitanashati

June 25, 2021 10:55 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link

Katika sehemu ya kwanza, mtoto wa Assane Diop, Raoul alitekwa na Leonard ambaye ni kibaraka wa bilionea Hubert Pellegrini ikiwa ni mtego wa kumvuta Assane katika umauti wake. Sehemu pili itakuaje? Picha| Tom’s Guide.


  • Baada ya mtoto wa Assane kutekwa, safari ya kumkomboa inaanza.
  • Mambo yanakuwa magumu baada ya polisi kuhusika.
  • Huenda ikawa ni mwanzo wa Assane kuanza kuwa baba ambaye Raoul anastahili.

Dar es Salaam. Kila mtu ana jambo ambalo analipambania. Familia, mali, furaha binafsi na wengine wanapambania umaarufu ili wajulikane. 

Wapo ambao mapambano yao ni zaidi ya mali na vitu vya kushikika. Ni mapambano ya maumivu yaliyoacha mioyo yao na damu inayovuja.

Hayo yote yanapatikana katika filamu ya “Lupin” sehemu ya pili ambayo inatikisa jukwaa la kutazamia filamu la Netflix. 

Katika sehemu ya kwanza, mtoto wa Assane Diop, Raoul alitekwa na Leonard ambaye ni kibaraka wa bilionea Hubert Pellegrini ikiwa ni mtego wa kumvuta Assane katika umauti wake.

Huenda Leonard hakufahamu uwezo wa ndege anayemvuta kwa mtama kwani Assane kama alivyo kasuku mjanja, amefanikiwa kunusa na kutegua mitego mingi.

Pale wawili hao wanapoongea katika simu, haya ndiyo yanayosikika: “Ukimuumiza mwanangu, nitakuua. Kama unamtaka mwanao, njoo umfuate,” ni majibizano kati ya Assane na leonard huku Raoul akiwa ndiye mtama wa kumvuta baba yake kikaangoni.

Watatu hao wapo katika jumba kubwa la kale ambalo liko nje kabisa na makazi ya watu. Leonard anatega mitego yake na kungojea usiku ambapo Assane atakuwa tayari kuanza mashambulizi.

Huenda ni kweli kila sungura ana kobe wake kwani katika mapambano hayo,  Assane anamzidi kete Leonard lakini hakufanikiwa kumkomboa mtoto wake.

Pale mlio wa simu yake unaposikika, ujumbe anaosoma “siku nyingine angalia kwenye gari” unampeleka dirishani ambako anaona gari la Leonard likiwaka moto huku likiwa na mwanaye Raoul ndani.

Ni simanzi, maumivu na msiba kwa Assane ambaye matendo yake yamefanya mtoto wake akutane na malaika mtoa roho. 

Hata wakati majonzi yakiendelea, Polisi wanafika na kumkamata Assane na safari ya kurudi Paris, inaanza. 

Mtuhumiwa huyo anaendelea kumlilia mtoto wake lakini pale polisi wanapomwambia kuwa hawakukuta mwili wa Raul kwenye gari, ni ishara ya mwanzo wa safari mpya yenye tabasamu kwa Assane.

Swali hapa ni Raul yuko wapi na yupo na nani? 

                       

Nilisahau kukuelezea hili. Wakati Assane anaenda kumkomboa mtoto wake baada ya kutekwa, aliongozana na Youssef Guidera, askari polisi ambaye alimdanganya Assane kuwa ni msamaria mwema anayetaka kumsaidia.

Kama umeona sehemu ya kwanza ya filamu hii unafahamu jinsi ilivyokuwa vigumu kumdanganya Assane kwani wanapofika katika gofu, ambalo Raoul yupo, Assane anamfungukia Guidera na kumwambia kuwa anafahamu kuwa yeye ni polisi na anafahamu kuwa mwanamama anayewasiliana naye aliyesema ni mke wake, ni polisi mwenzie ambaye yupo njiani anakuja.

Bila shaka umefahamu ninakoelekea. Kama bado, ninakufahamisha kuwa, Raul yupo na Guidera na aliokolewa naye kabla ya gari kuteketetea kwa moto.

Nisikunyime uhondo wa filamu hii lakini ninakuacha na maswali utakayoyajibu baada ya kuiangalia kwa njia ya mtandao.

Je, Assane atafanikiwa kutoroka katika mikono ya polisi?

Vipi kuhusu usalama wa Raul kwani licha ya kuwa katika mikono ya Guidera, Bado Pellegrini anamuwinda.

La mwisho ni je, kisasi cha Assane kwa mhasimu wake Pellegrini kitafanikiwa? Kazi ni kwako kuyatafuta majibu ya maswali hayo.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV