Ni ushindani: OnePlus yaingiza simu mpya sokoni
Skrini ya OnePlus ina ukubwa wa inchi 6.7, unaofaa kuiita simu kubwa. Picha| The Verge.
- Imetoa simu aina ya OnePlus ikiungana na Samsung Galaxy S22.
- Bei yake ni ndogo ikilinganishwa na OnePlus 9 Pro ya mwaka jana.
- Inauzwa kwa Sh2.1 milioni.
Dar es Salaam. Tangu mwaka uanze, ni simu mbalimbali za mfumo endeshi wa Android zimeingia sokoni. Nazungumzia Samsung na matoleo mengine.
Simu hizo zimeweka alama katika sekta ya matumizi ya betri, ubora wa kamera na teknolojia nyingine zinazobebwa na simu janja.
Kampuni ya kutengeneza bidhaa za kielektoroniki ya OnePlus haijachelewa kuungana na orodha hiyo baada ya kuingiza simu ambayo huenda bei yake haiumizi mfuko.
One Plus siyo ya “mchongo”
Bei ya simu hii siyo kubwa ikilinganishwa na toleo la 9 la mwaka jana. Kwa mujibu wa Shirika la habari la The Verge, simu hii inauzwa kwa Dola za Marekani 899 sawa takriban Sh2.1 milioni.
OnePlus 9 Pro ilitoka ikiwa na gharama ya Sh2.47 milioni, hivyo kwa bei hiyo, ni wazi kuna kama 300,000 ya kubakisha hapo ikilinganishwa na toleo la mwaka jana.
Skrini ya OnePlus ina ukubwa wa inchi 6.7, unaofaa kuiita simu kubwa. Urefu wa simu hii ni zaidi ya Samsung S22 na hata Pixel 6 Pro.
Kwa mujibu wa The Verge, skrini ya OnePlus 10 Pro haifikii ile ya Samsung Galaxy S22 hasa pale mtumiaji anapokuwa juani. Anayetumia Samsung atatumia simu yake bila shida kwani ina mwanga zaidi kuliko atakayetumia OnePlus.
Soma zadi
Kuna kazi inahitajika kwenye kamera
Kulikuwa na sifa nyingi kwa OnePlus upande wa kamera hasa baada ya kuungana na Hasselblad.
Kwa toleo hili, wadau wa kamera wamesema OnePlus anatakiwa kujifua.
Simu hii inaambatana na kamera tatu za nyuma na flashi ya nyuma. Kamera ya mbele imesasishwa na inapiga picha poa zaidi kuliko OnePlus 9 Pro.
Kamera kuu ina uwezo wa MP48, kamera ya mapana ina uwezo wa MP50 na kamera ya picha za karibu, ina uwezo wa MP8.
Mfumo wa kamera ni sawa sawa na wa OnePlus 9 Pro na haujabadilika. Kamera ya mbele ina uwezo wa MP32.
Kinahotakiwa kufanyiwa kazi ni uwezo wa kamera hii kupiga picha kwa muundo wa “RAW”, muundo ambao unamruhusu mtumiaji kuwa na udhibiti wa kamera yake.
OnePlus 10 Pro inaingia sokoni huku ikiwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Google Pixel 6.
Latest