Kuchelewa kulala kunavyoathiri utendaji wa kazi

September 15, 2018 12:35 pm · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Unapoteza uwezo wa kufanya maamuzi katika kazi zako za kawaida.
  • Hali hiyo huwa na athari katika utendaji wa ubongo wa binadamu ambapo inaweza kumpunguzia uwezo wake wa kibunifu na kufikiri
  • Unaweza kufa au kupata magonjwa ya moyo kwa kukosa usingizi wa kutosha.

Baadhi ya watu hudhani kwamba kulala usingizi ni kupoteza wakati. Wao huwa na shughuli nyingi za kibiashara na kirafiki kila siku, na hulala tu wanapokuwa wachovu sana. Kwa upande mwingine, wengine hutamani sana kupata usingizi wa uhakika matokeo yake humka wakiwa wachovu. 

Sababu zinazoathiri usingizi ni pamoja na matumizi ya pombe, madawa ya kulevya, vinywaji vyenye kafeini, kutumia simu kwa muda mrefu, kelele, kutokula mlo kamili, msongo wa mawazo.

Hali hiyo huwa na athari katika utendaji wa ubongo wa binadamu ambapo inaweza kumpunguzia uwezo wake wa kibunifu na kufikiri ili kutimiza malengo mbalimbali ya maisha. Athari kubwa ni kukosa kumbukumbu na kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo matatizo ya kukosa usingizi (insomnia).

“Mtu akikosa muda mrefu wa kulala anaweza hata kujisababishia kifo, kinachotokana na magonjwa ya moyo au presha” anasema Mtaalam wa Afya ya Akili wilaya ya Mbinga Dk Silvia Ngonyani.

Anabainisha kuwa ili kuepuka kulala muda mfupi na kunusuru uwezo wako wa ufanisi wa kazi ni vizuri kubadilisha mfumo wa utendaji na kupata muda upate muda wa kupumzisha akili.

Vilevile kupunguza matumizi ya simu za mkononi hasa nyakati za usiku, na kutafuta eneo tulivu la kulala kunaweza kurudisha hali yako ya kawaida ya kulala kwa kupumzisha mwili kama inavyotakiwa.


Zinazohusiana: 


Kupunguza tabia ya kufanya kazi muda mrefu ili  kuruhusu  mwili kupata hali ya kupumzika kwasababu ukilinganisha na mtu ambaye anafanya kazi kwa masaa machache utaona jinsi anavyokuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kufanya jambo kutokana na kupata muda wa kupumzika.

Ukosefu wa usingizi wa kutosha unaathiri utendaji wa mwili. Picha| Sutter Health

Hii inatuleta katika ule mfumo uliozoeleka wa kufanya kazi kwa masaa nane kwa siku na 40 kwa wiki, lakini unajua kufanya kazi masaa nane ilipotokea?

Ilianzia huko Marekani baaada ya utafiti wa mwanzilishi wa Kampuni ya Ford Motor, Henry Motor mwaka 1926 kugndua uzalishaji unapungua katika kampuni yake. Akupunguza muda wa kazi kwa wafanyakazi wake toka masaa 10 hadi nane na kutoka siku sita hadi tano ili wapate muda mrefu wa kupumzika na hapo ufanisi wa uzalishaji katika kiwanda chake ukaongezeka.

Hivyo hiyo, hiyo moja ya njia inayokuonyesha kama ukipata muda mrefu wa kupumzika unaweza kuwa na uwezo zaidi wa kufikiria kuhusu mawazo mapya na kuongeza utendaji wako wa kazi.

“Watu hawajui athari za kulala masaa machache kwasababu madhara yake huja baada ya muda mrefu,” anasema Mtaalam wa Magonjwa ya Usingizi kutoka Chuo Kikuu cha Chicago, David Gozal.

Hivyo ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha anapata usingizi wa kutosha kuepuka madhara ya kukosa usingizi uhakika, huku wataalam wakishauri kuhakikisha unafanya mazoezi ya kutosha na kuzingatia muda wa kulala kwa afya bora.

Enable Notifications OK No thanks