Kigogo TANROADS ateuliwa kuiongoza TAA

March 26, 2019 9:02 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni Mhandisi Julius Ndyamukama aliyekuwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Dar es Salaam.
  • Pia alikuwa msimamizi mkuu wa ujenzi wa jengo jipya namba 3 (Terminal 3) la uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) ambayo yako katika hatua za mwisho kukamilika.  

Dar es Salaam. Rais  John Magufuli amemteua Mhandisi Julius Ndyamukama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). 

Mhandisi Ndyamukama anachukuwa nafasi ya Richard Mayongela ambaye uteuzi wake umetenguliwa na anatakiwa kuripoti Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano arnbako atapangiwa kazi nyingine. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kabla ya uteuzi huo Mhandisi Ndyamukama alikuwa Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Dar es Salaam na ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa ujenzi wa jengo jipya namba 3 (Terminal 3) la uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) ambayo yako katika hatua za mwisho kukamilika.  

Uteuzi wa Mhandisi Ndyamukama unaanza leo Machi 26, 2019.


Soma zaidi: 


Ujenzi wa jengo hilo unatekelezwa na kampuni ya Bam International ya Uholanzi ikisaidiwa na kampuni nyingine takribani 21 za ndani na nje ambapo ujenzi huo ulianza mwaka 2013 na unakusudiwa kukamilika mwaka huu kwa gharama ya Sh560 bilioni.

Jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege 17 hadi 19 zikiwemo kubwa kwa wakati mmoja na kumudu abiria milioni 6 kwa mwaka ambapo katika eneo la nje ya uwanja kuna nafasi ya kuegesha magari 2,000 ya watu wanaotumia uwanja huo.

Enable Notifications OK No thanks