Wageni shughuli za kidini, kujitolea vinara kukaa muda mrefu Tanzania

March 26, 2019 1:11 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanatumia wastani wa siku 12 ambapo ni juu kidogo ya muda wanaokaa wageni wote wa wastani wa siku 10.
  • Wageni wanaokuja kwa shughuli za kibiashara wanatumia muda mchache zaidi kukaa nchini. 

Dar es Salaam. Licha ya Tanzania kuwa na vivutio vingi vya utalii, bado idadi ya wageni wanaokuja kwa shughuli za kidini na kujitolea wanaongoza kukaa muda mrefu zaidi ukilinganisha na shughuli zingine ikiwemo mapumziko, starehe na kutembelea ndugu na marafiki. 

Kwa wastani wageni wanaoingia Tanzania kwa shughuli za kidini na kujitolea hutumia siku 12 (12 nights) kukaa nchini ambazo ni nyingi zaidi ukilinganisha na wageni wanaokuja kwa shughuli zingine.  

Ripoti ya utafiti ya wageni wa nje ya nchi mwaka 2017 (International Visitors’ Exit Survey Report 2017) iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaeleza kuwa wastani wa wageni waliotembelea Tanzania hutumia siku 10 kukaa nchini na hali hiyo imedumu kwa takribani miaka sita iliyopita. 

Licha ya wageni wote kutumia wastani wa siku 10 kukaa nchini tangu mwaka 2012, wageni wanaokuja kwa shughuli za kidini na kujitolea wako juu ya wastani wa siku wanazotumia wageni wote. 

Mathalani, mwaka 2017 wageni wote walikaa kwa wastani wa siku 10 ikiwa ni pungufu kidogo na siku 11 walizokaa mwaka 2016. Mwaka 2015 wageni hao walikaa nchini kwa wastani wa siku 12.  

Hali hiyo ni tofauti kidogo na muda wanaotumia wageni wanaokuja kwa ajili ya mapumziko na kustarehe katika maeneo mbalimbali ya utalii. Mwaka 2017 wageni hao walitumia wastani wa siku 11 ikiwa ni chini kidogo ya wale waliokuja kwa shughuli za kidini na kujitolea. 

Katika kipindi hicho cha mwaka 2017, wageni waliokuja kwa shughuli za kibiashara ndio walirekodiwa kiwango kidogo kabisa cha siku wanazokaa nchini ambapo walitumia wastani wa siku nane tu.

Licha ya kutofautiana kwa muda wa kukaa kwa wageni wanaokuja nchini, Waholanzi walikaa muda mrefu zaidi kwa wastani wa siku 14 wakifuatiwa na Waingereza kwa siku 13. 


Zinazohusiana: 


Mataifa mengine ambayo wananchi wake walikaa muda mrefu ni pamoja na Marekani, Ujerumani, Uswisi, Canada na Australia huku wageni kutoka Kenya na Afrika Kusini wakitumia muda mchache zaidi kukaa nchini ambapo wengi wao walikuja kwa shughuli za kibiashara. 

Ripoti hiyo inaeleza kuwa juhudi zaidi zinahitajika katika kuweka mazingira mazuri ya ukuaji wa sekta ya utalii ili kuongeza muda wa watalii wanaotumia kukaa katika maeneo ya utalii. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
19 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
19 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV