Serikali imesema imeajiri walimu zaidi ya 14,000 ndani ya miaka miwili

June 3, 2019 8:00 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Mbunge  wa jimbo la  Madaba, Joseph Mhagama amehoji kwanini Serikali isiwe inasomesha walimu kulingana na mahitaji ya soko.
  • Serikali imesema imeajiri walimu 14,422 ndani ya miaka miwili ya hivi karibuni.

Dar es salaam. Serikali imesema imeajiri walimu 14,422 ndani ya miaka miwili ya hivi karibuni huku ikieleza kuwa haitasita kusomesha wanafunzi wanaosomea taaluma ya ualimu licha ya kuwa wengi ili kuwapatia wigo mpana wa fursa za ajira na kujiajiri. 

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais- Tamisemi Mwita Waitara ameeleza leo bungeni kuwa kati ya walimu hao waliojiriwa kati ya mwaka 2017/18 na 2018/19, takriban robo tatu au walimu 10,695 waliajiriwa shule za msingi na 3,727 waliosalia wanafundisha shule za sekondari. 

Waitara alikuwa akijibu swali ya mbunge wa Mbinga, Martin Msuha aliyetaka kufahamu  mkakati wa Serikali kupeleka walimu wa masomo hayo wilayani Mbinga baada ya kuwepo uhaba wa walimu wa hisabati na sayansi uliyoathiri zaidi zaidi matokeo ya masomo hayo. 

Akijibu swali hilo, Waitara amesema zipo sababu nyingi zilizosababisha kushuka ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba wilaya ya Mbinga ikiwemo upungfu wa walimu, utoro na ushiriki hafifu wa wazazi katika kufutilia masomo ya elimu ya watoto wao.


Zinazohusiana:
Shule zinavyochuana kubaki katika 10 bora kidato cha sita


“Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imepatiwa walimu 143 ambapo  walimu 112 ni wa  shule msingi na walimu 31 wa shule za  sekondari,’’  amesema Waitara wakati akielezea mgawanyo wa walimu waliopelekwa Mbinga katika kipindi cha miaka miwili ya hivi karibuni. 

Hata hivyo, katika swali la nyongeza Mbunge  wa jimbo la  Madaba, Joseph Mhagama amehoji kwanini Serikali isiwe inasomesha walimu kulingana na mahitaji ya soko badala ya inavyofanya sasa ambapo vijana wengi waliosomea ualimu wapo mtaani. 

“Tunaendelea na mchakato  wa kuhakikisha wanafunzi hao badala ya kutegemea kuajiriwa tu na Serikali bali kuona watakavyoaanzisha kufanya kazi hata kwa shughuli binafsi,” amesema Waitara. 

aitara amesema ni kweli kuna walimu wengi  mtaani lakini ni kweli tunahitaji walimu katikshule zote za msingi na sekondari

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV