Deni la Serikali laongezeka kwa asilimia 2.3, lafikia Sh51 trilioni

June 3, 2019 2:13 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Dk Mpango amesema tathmini inaonyesha bado ni himilivu.
  • Ongezeko la deni hilo limechagizwa na ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo likiwemo jengo la tatu la Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere. 

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesea deni la Serikali limeongezeka kwa asilimia 2.3 ndani ya mwaka mmoja kutoka Sh49.86 trilioni Aprili 2018 hadi Sh51.03 trilioni Aprili mwaka huu likichagizwa zaidi na uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye miradi ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa. 

Kati ya kiasi hicho, Dk Mpango amesema deni la ndani ni Sh13.25 trilioni wakati lile la nje ni Sh37.78 trilioni.

“Ongezeko la deni la Serikali lilinatokana na kupokelewa kwa mikopo mipya kwa ajili ya kugharamia miradi mipya ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa jengo la tatu la Kiwanja cha Kimataifa wa Julius Nyerere, ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa, ujenzi wa miradi ya umeme na ujenzi wa madaraja makubwa na barabara,” amesema Dk Mpango bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake. 

Mtaalamu huyo wa uchumi amesema matokeo ya tathmini iliyofanywa Desemba mwaka jana inaonyesha deni la Taifa ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.

Dk Mpango amesema uwiano wa thamani wa sasa wa deni la Taifa kwa pato la Taifa (Present value of total public debt) ni asilimia 27.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 70. 


Zinazohusiana: 

“Thamani ya sasa ya deni la nje pekee kwa pato la Taifa (Present value of external debt) ni asilimia 22.2 ukilinganishwa na ukomo wa asilimia 55,” amesema na kuongeza;

“Thamani ya sasa la deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 157.3 ikilinaginsihwa na ukomo wa asilimia 240 na ulipaji wa deni la nje kwa kutumia mauzo ya bidhaa nje ni asilimia 15.2 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 23.”

Amesema katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, Serikali ilitenga Sh1.41 trilioni kwa ajili ya kulipa riba ya deni la ndani na kwamba hadi Aprili mwaka huu Sh1.06 trilioni ilikuwa imeshalipwa sawa na asilimia 75.2 ya lengo. 

Katika kuhudumia deni la nje, Dk Mpango amesema Serikali ilitenga Sh689.67 kwa ajili ya kulipa riba ya deni la nje na hadi Aprili 2019 Sh588.3 bilioni ikiwa ni sawa na asilimia 85.3 ya lengo hilo.

“Wizara itaendelea kusimamia Deni la Serikali kwa kuzingatia Sheria ya mikopo, dhamana na misaada SURA 134 pamoja na Mkakati wa Muda wa kati wa Kusimamia madeni,” amesema. 

Baadhi ya wabunge wameonyesha hofu juu ya ongezeko hilo deni hili na kushauri Serikali idhibiti ili liendelee kuwa stahimilivu.

“Wito wangu ni kwa ziara ni kuangalia kuwa deni hili liendelee kuwa stahimilivu. Ukiangalia sasa zaidi ya trilioni 50 wakati sisi uwezo wetu wa kukusanya mapato ya ndani ya zaidi ya trilioni 20 kidogo linakuwa na mashaka hasa kwa sisi ambao siyo wachumi,” amesema Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Justine Monko na kuongeza;
“Wizara itupie macho katika deni la Taifa na kuangalia tusije tukateleza.” 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV