Viongozi, wananchi watakiwa kuitekeleza bajeti ya 2019-2020 kwa vitendo

June 29, 2019 9:49 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akiahirisha Bunge siku ya jana. Picha|Ofisi ya Waziri Mkuu.


  • Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema utekelezaji wa bajeti hiyo unategemea nidhamu na utashi wa viongozi na wananchi.
  • Wametakiwa kuwaongoza wananchi kulinda miundombinu inayojengwa na Serikali. 
  • Washirika wa maendeleo waombwa kuchangia katika utekelezaji wa bajeti. 

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka viongozi na watendaji wa Serikali katika ngazi zote kuwajibika ipasavyo na kudumisha nidhamu katika utekelezaji wa majukumu ili kuwezesha utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2019/2020. 

Serikali imepanga kutumia Sh33.11 trilioni ambapo Sh20.86 trilioni zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida sawa na asilimia 63 ya bajeti yote. 

Amesema ili kufikia lengo na dhamira ya kutekeleza mipango ya maendeleo na bajeti ya Serikali ya 2019/2020 kwa ufanisi, viongozi hao wanatakiwa waendelee kuwasisitiza wananchi kushiriki ipasavyo kulinda miundombinu inayojengwa katika maeneo mbalimbali nchini. 

Waziri Mkuu alikuwa akizungumza jana (Juni 28, 2019) wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa Bunge, jijini Dodoma litakalorejea tena Septemba 3 mwaka huu.


Zinazohusiana: 


Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania pamoja na washirika wa maendeleo waiunge mkono Serikali katika kutekeleza vipaumbele vilivyowekwa kwenye bajeti ya mwaka 2019/2020 ili viweze kutoa mchango wa haraka katika maendeleo ya uchumi na ya watu.  

Vipaumbele vinakusudiwa kutekelezwa katika bajeti hiyo ni pamoja na miradi ya viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi nchini; kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu; uboreshaji wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji: na kuimarisha zaidi ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika ngazi zote.

Katika hatua nyingine, Majaliwa amezitaka mamlaka husika zishirikiane na wadau katika kudhibiti uharibifu wa mazingira kwa kukomesha ukataji hovyo wa misitu, uchafuzi wa bahari, mito na maziwa na taka za plastiki ili kulinda mazingira asilia.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV