Facebook kuanza kuwachaguliwa wafuasi wake viongozi wa makundi

July 16, 2019 11:55 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Itakuwa inachagua kwa kutumia kipengele hicho kipya cha waongoza makundi kinachojulikana kama ‘Suggested Moderators’.
  • Viongozi watakaochaguliwa watapimwa wa ushiriki wao kwenye mijadala ya kundi husika.
  • Wataalam wa mitandao ya kijamii wapinga hatua na kusema ni kuminya uhuru wa wafuasi wa Facebook.

Katika kuhakikisha inadhibiti na kuboresha mtandao wake, Facebook imeanza kufanya mchakato wa kuteua viongozi wanaotakiwa kuongoza makundi mbalimbali ya mtandao huo. 

Baadhi ya wataalamu wa mitandao ya kijamii, wamesema hatua hiyo ni kuminya uhuru wa wafuasi wake na kuwa hatua hiyo huenda isifanikiwe. 

Facebook imeanza majaribio ya kipengele hicho kipya cha waongoza makundi kinachojulikana kama ‘Suggested Moderators’  ambacho kimeanza kutumika katika baadhi ya makundi. 

Kupitia kipengele hicho, mifumo ya Facebook ya usomaji taarifa za wachangiaji kwenye makundi, kitaweza  kupendekeza mjumbe yeyote kuwa kiongozi wa kundi husika hata kama lina mwanzilishi wake. 

Uteuzi wa kiongozi wa kundi utategemea mchango wake na jinsi anavyojihusisha na mijadala ya kundi. 

Hata hivyo, baadhi ya watu wamesema hatua hiyo ya Facebook haitaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa sababu maudhui na madhumuni ya makundi yanatofautiana kimtazamo.


Zinazohuiana: Facebook yafanya maboresho utafutaji wa bidhaa mtandaoni.


Tovuti ya social media unaondika habari za msuala ya mtandao ya kijamii umesema haitawezekana mfanyabishara kumpa ruhusu mtu asiyemjua aongoze kundi analotumia kutangaza bidhaa au huduma.

Tovuti hiyo imesema kipengele hicho kinaweza kufanya kazi labda kwenye makundi ya kijamii ambayo hayana shughuli za kibiashara. 

Maoni mengine yametolewa katika ukurasa wa Twitter wa @MattNavarra ambapo yanaeleza kuwa, tayari ninacho hicho kipengele kwenye kompyuta yangu (desktop) ni hatari kumpa mtu uongozi wa kundi kwa kuangalia utendaji wake kwenye hilo kundi,”

Enable Notifications OK No thanks