Usafiri wa ndege unavyoweza kukutanisha na mwenza wa maisha

September 3, 2019 6:00 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Lakini kama unataka kuonana na mtu umtakaye kwenye ndege, zipo programu tumishi zinazoweza kukuunganisha na mtu uliyemkusudia. Picha|Mtandao.


  • Utafiti uliofanyika hivi karibuni unaeleza kuwa mtu mmoja kati ya 50 anaweza kupata mwenza wa maisha akiwa kwenye ndege.
  • Hilo linawezekana kama msafiri ataanzisha mazungumzo na mtu anayeona anamfaa.
  • Pia programu tumishi kama Planely na btrfly zinaweza kukuunganisha na marafiki ukiwa kwenye ndege.

Dar es Salaam. Usafiri wa ndege siyo tu unakuwezesha kulifikia eneo unalokwenda kwa urahisi, bali ni sehemu muhimu ya kukufungulia fursa mbalimbali ikiwemo za kibiashara na hata mahusiano yanayopelekea kumpata mwenza wa maisha. 

Utafiti mpya uliofanywa na benki ya HSBC yenye makao makuu nchini Uingereza kuhusu wasafiri wanaotumia ndege umeeleza kuwa mtu mmoja kati ya 50 anayetumia usafiri huo amekuwa akipata mwenza wa maisha kwa kuanzisha mazungumzo akiwa ndani ya ndege.  

 Utafiti huo ambao uliwahoji watu 5,000 waliosafiri kwa kutumia ndege kutoka nchi 141 duniani ulifanyika July 2018, amesema watu waliohojiwa wameeleza kuwa kama mtu ataanzisha mazungumzo na watu kwenye ndege ana uwezekano wa kupata fursa mbalimbali ikiwemo mwenza wa maisha. 


Inayohusiana:


Pia ulibaini kuwa asilimia 16 ya wasafiri walitengeneza muunganiko wa kibiashara wakiwa kwenye ndege, huku asilimia 14 walipata fursa ya kujenga urafiki wa kudumu na watu waliokutana nao kwa mara ya kwanza. 

Kama wewe ni mtu unayependa kuanzisha mahusiano na kupata marafiki wenye faida hata kupata mwenza wa maisha, basi ukiwa kwenye ndege anzisha mazungumzo na jirani yako uliyekaa naye.

Lakini kama unataka kuonana na mtu umtakaye kwenye ndege, zipo programu tumishi zinazoweza kukuunganisha na mtu uliyemkusudia. 

Programu ya btrfly inakuunganisha na wasafiri katika viwanja vya ndege 380 duniani ikiwa utaweza taarifa zako za ndege au kiwanja cha ndege unachotumia. 

Pia programu ya Planely inayofanya kazi kama mtandao wa kijamii, unawaunganisha wasafiri wa ndege kulingana na vitu wanavypendelea wakiwa kwenye ndege au wakati wakisubiri kupanda ndege. 

Enable Notifications OK No thanks