Motorola Razr:Simu inayogharimu zaidi ya Sh3.4 milioni
- Imezinduliwa Novemba 13, 2019.
- Muundo wake unafanana na razr ya mwaka 2004.
- Haina teknolojia ya redio.
Dar es Salaam. Kama ulikuwa mdau wa simu za Motorola miaka 15 iliyopita basi muundo wa Motorola Razr ya mwaka 2019 umerudi lakini safari hii kwa muundo tofauti na ule wa Motorola Razr v3 ya mwaka 2004, kwa uwezo na muonekano lakini muundo unakaribiana.
Razr V3 ambayo ukubwa wa skrini yake ni inchi 2.2 huku uwezo wa betri yake ukiwa ni mAh680 na uhifadhi wake ukiwa ni MegaBaiti (MB) 5 hadi MB13 kwa sasa inagahrimu chini ya Sh231,000.
Kwanini yaongelewe ya kale? Mbali na kuwa na skrini mbili, hizi ndizo sababu nyingine za Razr 2019 inayotumia mfumo endeshi wa Android kuuzwa zaidi ya Sh3.45 milioni.
Uhifadhi
Simu ya Razr 2019 ya Motorola ina uwezo mkubwa kwenye uhifadhi wa ndani yaani “internal storage” kwa kuwa na ukubwa wa GB 128 huku uwezo wa uhifadhi wa muda yaani RAM ni GB 6 ambayo ni kubwa kwa mujibu wa wadau mbalimbali wakiwemo Emanuel Evans ambaye ni mtengeneza programu.
Kwa ngazi ya uhifadhi, simu hii inakuja na uwezo wa kuhifadhi picha na video za kwenye simu yako kwa mfumo Automatiki kwenye “back up” ambayo inaweza kupatikana kwenye kifaa cha kielektroniki chochote. Haya ni maboresho makubwa kutoka kutoka Mb13 za uhifadhi hadi GB 128 na zaidi.
Muundo wa Motorola Razr ya mwaka 2019 umerudi tena lakini safari hii kwa muundo nitofauti na ile Motorola razr v3 ya mwaka 2004. Picha| Motorola.
Betri
Likini kwa upande mwingine ukubwa wa betri simu hii mAh2510 ikiwa ni uwezo mdogo ukilinganisha na simu janja zingine zinazoshindana kwenye soko kama Samsung S10 yenye betri yenye ukubwa wa mAh 3400 na I phone 11 ambayo betri yake ina ukubwa wa mAh 3969
Kamera
Kwa kutumia simu hii, mtumiaji anaweza kupiga picha na kurekodi video vizuri kwa kutumia kamera yenye ukubwa wa Megapikseli (MP) 16 ambayo ni sawa na Samsung S10 vilevile ni zaidi ya Iphone 11 pro yenye ukubwa wa MP 12.
Hata hivyo, ukikunjua simu hiyo, uwezo wa kamera yake unapungua unakuwa mdogo ukilinganisha na simu zinazochuana sokoni kwani ukubwa wa kamera yake ya mbele (selfie camera) ni MP5.
Hata hivyo, mtumiaji wa simu hii anauwezo wa kuchagua kupiga “Selfie” kwa kamera ya mbele (simu ikikunjuliwa) au kamera ya nyuma (Simu ikikunjwa)
Kamera yake inakuja na teknolojia ya “auto focus” ikiambatana na flashi 2 ambazo zinampatia mtumiaji wa simu hiyo uwezo wa kupiga picha za “potrait”.
Zinazohusiana
- Samsung, Huawei zinavyochuana katika soko la simu duniani
- Sifa za simu mpya za Samsung zilizoingia sokoni Agosti 7
Skrini
Simu hii ina skrini mbili yaani skrini kubwa ambayo inaonekana pale inapokunjuliwa na skrini ndogo ambayo inaonekana simu ikikunjwa. Skrini ndogo inamuwezesha mtumiaji kujibu meseji, kusikiliza muziki kwa kupeleka mbele ama kusimamisha muziki na kurudisha nyuma.
Mbali na hayo, skrini ndogo inaonyesha saa na “notification” zote za simu na hivyo kutompa ulazima mtumiaji kuikunjua kwa matumizi madogo madogo.
Ukubwa wa Razr 2019 ikikunjuliwa kwa “Display” ni inchi 6.2” ambazo zinakunjika. Teknolojia ya Display hiyo ni ya sinema (21:9 Cinemavision) yenye uwezo wa HD (2142 x 876p). Ikikunjwa, simu hiyo skrini ndogo yenye ukubwa wa inchi 2.7.

Mtumiaji wa simu hii anauwezo wa kuchagua kupiga “Selfie” kwa kamera ya mbele (simu ikikunjuliwa) au kamera ya nyuma (Simu ikikunjwa). Picha| Motorola.
Mengineyo
Simu hii ina maiki 4 na kwaajili ya usalama, inatumia teknolojia ya alama za vidole na nyiwila (password) kuifungua. Pia Razr inaweza kuhimili unyevu na maji kiasi cha mtu kuweza kuitumia kwenye mvua ya kawaida.
Upekee mwingine wa simu hii ya Razr ya 2019 ni kuwa inatumia kichajio aina ya “type C” na “earphones” zake zina teknolojia ya “noise cancellation”
Hata hivyo, cha kusikitisha kuhusiana na simu hii ni kwamba haina redio na wadau wengi wa simu wanajiuliza kama haitakuwa “yai” kwa maana ya kwamba ihitaji uangalifu mkubwa kwa mtumiaji kwani ni nyembamba.
Endelea kusoma www.nukta.co.tz kwa habari za teknolojia zinazoshika masikio ya watu.
Latest