Zingatia haya unapofanya manunuzi siku ya “Black Friday”

November 25, 2019 1:47 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Kwa mwaka 2019, itafanyika Novemba 29.
  • Ni siku mahususi ya promosheni ya bei ya maduka makubwa.
  • Zingatia bajeti na ubora wa bidhaa kabla ya kufanya manunuzi.

Dar es Salaam. Kila ufikapo mwezi Novemba, matangazo ya “Black friday” hufurika mitandaoni ikiashiria promosheni za manunuzi ya bidhaa na vitu mbalimbali kwenye maduka zimeanza.

Kwa kawaida, “Black friday” hufanyika siku moja baada ya sikukuu ya shukurani (Thanks giving) ambayo inasherehekewa nchini Marekani na Canada kwa ajili ya mavuno na baraka zingine ambazo wamezipata kwa mwaka ulioisha.

Black Friday  ni muda maalumu ambapo maduka hufunguliwa wakati wa jioni na bidhaa huuzwa kwa bei ya chini mno kuliko mteja anavyotarajia. Wamarekani wamekuwa wakiitumia siku hii kununua bidhaa ambazo zinaashiria kuanza kwa maandalizi ya zawadi za Krismas na kufunga mwaka.

Kwa mwaka huu wa 2019, Black Friday imeangukia Novemba 29 huku matangazo ya mtandaoni ya makampuni mbalimbali ya manunuzi yakiwemo ya DHL na Easy Buy Africa yakiwa yameanza kuwekwa mtandaoni. 

Upekee wa siku hiyo ni kuwa maduka mengi huweka punguzo la bei ili kuvutia wateja wengi zaidi hasa kufanya manunuzi ya msimu wa sikukuu za Krismas na mwaka mpya.

Siku hiyo haiwahusu Wamerekani pekee, bali hata watu wengine duniani. Huhitaji kuwa na haraka ya kufanya manunuzi kwani unatakiwa kujipanga ili kuepuka kujuta hapo baadaye. Uzingatie nini kwenye Black Friday?

  1. Umakini mtandaoni

Katika kufanya manunuzi ya mtandaoni ni muhimu kuwa na uhakika na duka ambalo unafanya manunuzi hayo ili kuepuka kupoteza pesa zako kwani maduka mengine ni maduka hewa.

Tambua tovuti rasmi za maduka ya mtandaoni ili kuepuka “kuingia mkenge” kwani katika msimu huu, baadhi ya wadukuzi hutengeneza tovuti feki kwa ajili ya kuiba fedha kwa njia ya mtandao.


Zinazohusiana:


  1. Tenga bajeti yako

Kutokana na bidhaa nyingi kuuzwa kwa bei ya punguzo, unaweza kujikuta unanunua vitu hata ambavyo haukuwa na mpango navyo. Ni muhimu kuweka bajeti yako na kisha kuandaa orodha ya vitu unavyovihitaji zaidi.

Mfano, kama unahitaji vitu vya nyumbani, ni vema kuweka vipaumbele kwenye bidhaa ambazo zinakuwa na muhimu kuliko vingine.

Black Friday  ni muda maalumu ambapo maduka hufunguliwa wakati wa jioni na bidhaa huuzwa kwa bei ya chini mno kuliko mteja anavyotarajia na watu hutumia siku hiyokununua bidhaa kwa ajili ya maandalizi ya zawadi za Krismas na kufunga mwaka. Picha|Mtandao.

  1. Linganisha bei

Ni msimu wa punguzo, hivyo kila duka huweka bei itakayovutia wateja wengi zaidi. Usiwe na haraka bali chukua muda na tembelea maduka mawili matatu kulinganisha thamani ya bidhaa unazozihitaji.

Baada ya kufanya hayo, sasa unaweza kufanya maamuzi ni wapi ununue kipi na wapi usirudi tena.

  1. Nunua vifaa vipya

Unaweza kukutana na bidhaa ambazo siyo imara katika msimu huu wa promosheni na hiyo inaweza kukupotezea pesa zako kwa kunua vifaa vitakavyoharibika kwa muda mfupi. Usidanganywe na bei, angalia ubora wa vifaa na bidhaa ndipo ununue bidhaa ambayo haitakufanya ujute hapo mbeleni. 

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW