Petroli, dagaa zachangia kushusha mfumuko wa bei Januari

February 10, 2020 11:14 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Januari 2020, umeshuka hadi kufikia asilimia asilimia 3.7 kutoka 3.8 iliyorekodiwa katika mwaka ulioishia Disemba 2019.
  • Imechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini Tanzania kwa mwezi Januari 2020, umeshuka hadi kufikia asilimia asilimia 3.7 kutoka 3.8 iliyorekodiwa katika mwaka ulioishia Desemba 2019 ikichangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula ikiwemo dagaa na petroli.

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

“Mfumuko wa bei kwa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Januari umepungua hadi asilimia 5.7  kutoka asilimia 6.3 kwa mwaka ulioisha mwezi Disemba, 2019, ” inasomeka sehemu ya ripoti ya mfumuko wa bei ya NBS iliyotolewa leo (Februari 10, 2020).

NBS imesema kuwa baadhi ya bidhaa za chakula zilizochangia kupungua kwa kasi ya bei kwa mwezi Januari 2020 ikilinganishwa Januari 2019 ni pamoja na dagaa kwa asilimia 1.4 na viazi asilimia 3.4.

Ukiondoa dagaa na viazi bidhaa nyingine ambazo kasi ya mfumuko wa bei imepungua ni magimbi kwa asilimia 7.1 na ndizi za kupika kwa asilimia 2.8. 


Zinazohusiana: 


Kwa upande wa bidhaa zisizo za chakula zilizopungua bei kwa mwezi Januari, 2020 ikilinganishwa na bei za mwezi  Januari 2019 ni pamoja na gesi kwa asilimia mbili, mafuta ya taa asilimia 4.6, petroli asilimia 1.5, dizeli kwa asilimia 1.3 na majiko ya gesi kwa asilimia 4.6.

Bidhaa hizo hutumika karibu kila kaya nchini kutokana na umuhimu wake kwenye maisha ya kila siku na pia ni chanzo cha kipato kwa wanaojishughulisha na usafirishaji na kilimo cha mazao hayo.

Hata hivyo, mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki. Kwa mwaka unaoishia Januari 2020, Kenya umeshuka hadi asilimia 5.78 kutoka asilimia 5.82 kwa mwaka ulioishia Desemba, 2019. Uganda nako umeshuka hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioisha mwezi Desemba, 2019.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV