“Startups” zaanza kutumia fursa iliyoachwa na Jumia Tanzania

March 2, 2020 3:49 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Zaanza kufungua maduka ya mtandaoni kutoa huduma kama za Jumia.
  • Zapania kuzifanyia kazi changamoto za muda na usambazaji wa bidhaa kwa wateja. 

Dar es Salaam. Huenda ukawa mmoja ya wapenzi wa kutumia maduka ya  mtandaoni kuagiza  na kununua bidhaa mbalimbali unapokuwa umetingwa au ukiwa katika mapumziko nyumbani.

Huduma hizi ni msaada mkubwa pale mtu anapokosa muda wa kwenda dukani, sokoni au hata hotelini kupata huduma mbalimbali anazozihitaji kwa muda muafaka.

Licha ya baadhi ya kampuni zinazoratibu biashara ya bidhaa na huduma mtandaoni ikiwemo ya Jumia kuondoka Tanzania kutokana na sababu mbalimbali, imeibuka kampuni nyingine ambayo inatoa huduma kama za Jumia.

Huenda ulikuwa unawaza baada ya Jumia, nani ataingia sokoni kukupa kile unachotaka, basi tovuti ya kuagiza na kununua bidhaa mtandaoni ya Piki  inaweza kuwa imebeba majibu yako. 

Piki iliyoanzishwa takriban wiki mbili zilizopita na vijana wa Tanzania,  inamwezesha mtu kuagiza bidhaa mbalimbali kama chakula, vifaa vya nyumbani, vifaa vya kielektroniki na vinywaji mtandaoni na kuletewa mahali popote kwa muda mfupi.                                                                                              

Utaweza kupata huduma zote hizo kwa kutumia simu janja, tableti, na kompyuta hasa katika majiji makubwa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha baada ya kuainisha eneo ulipo na kukubaliana na bei ya bidhaa husika. 

Piki imekuja na maboresho mbalimbali ikiwemo kuongezwa kwa huduma ya usambazaji wa vifaa vya nyumbani, vifaa vya kielektroniki na vinywaji ambavyo viko mbali na chakula tofauti na ilivyokuwa kwenye “Jumia Food”.

Piki pia imefanya maboresho ya muda utakaomchukua mteja au mtu aliyeagiza bidhaa kusubiri mzigo wake anapokuwa ameagiza. Badala ya mzigo kumfikia mlengwa baada ya siku tatu ilivyo kwa kampuni nyingine, mteja anapata mzigo wake baada ya nusu saa.


Zinazohusiana:


Kwa sasa, huduma hiyo inapatikana kwenye simu zenye mfumo wa Android na inategemea kujitanua kwenda kwenye mfumo wa iOS mwishoni mwa wiki hii. 

Mmoja wa waanzilishi wa tovuti hiyo, Emmanuel Charles ameiambia www.nukta.co.tz kuwa wanakusudia kuhakikisha mtandao wao unakuwa na kasi hasa katika kuimarisha mifumo ya usambazaji bidhaa kwa wateja baada ya kuagiza. 

“Kwenye Jumia ilikuwa inamchukua mteja siku tatu kupata bidhaa ya kielektroniki aliyoagiza, kwa sasa hivi mteja anapoagiza simu au kifaa chochote anakipata ndani ya nusu saa,” amesema Charles.

Ili kuhakikisha wanawafikia wateja wanaogiza bidhaa kwa muda mfupi, wanawatumia wasambazaji wao wa bidhaa ambao wako karibu na maeneo ambayo wanaishi wateja. 

Hata hivyo, Piki itakuwa na kibarua kigumu kuhakikisha huduma zake zinakuwa endelevu ikizingatiwa kuwa bado kuna changamoto kwa Watanzania kuchangamkia fursa za mtandaoni. 

Jumia ilifungasha virago vyake na kuondoka Tanzania Novemba 27, 2019 kwa madai kuwa inaangazia masoko sehemu nyingine duniani.

Baadhi ya wataalam na wachambuzi wa masuala ya biashara waliambia  www.nukta.co.tz kuwa zipo sababu nyingi zinazosababisha kampuni zinazoendesha biashara ya mtandaoni sifanikiwe ikiwemo uelewa mdogo kuhusu masoko na elimu ya juu ya teknolojia ya mifumo ya kidijitali bado ni changamoto kwa Watanzania wengi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV