Bei ya mahindi yaleta tofauti Lindi, Mara

March 18, 2020 11:37 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Gunia la kilo 100 la mahindi linauzwa kwa Sh120,000 katika Mkoa wa Lindi wakati Mara linauzwa Sh45,000.
  • Wafanyabiashara wa Lindi huenda wakafaidika maradufu kuliko wale wa Mara.

Huenda wafanyabiashara wa mahindi katika Mkoa wa Lindi leo wataneemeka kwa mauzo mazuri baada ya mkoa huo kurekodi bei ya juu ya zao hilo ikilinganishwa na maeneo mengine nchini Tanzania.

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara leo (Machi 18, 2020) zinaonyesha kuwa gunia la kilo 100 la mahindi linauzwa kwa Sh120,000 katika Mkoa wa Lindi. 

Bei hiyo inayotumika katika masoko ya mkoa huo ndiyo bei ya juu kabisa nchini Tanzania, jambo linalowafaidisha wafanyabiashara waliopeleka zao hilo katika mkoa huo wa kusini mwa Tanzania. 

Hata hivyo, wenzao wa Musoma mkoani Mara guni hilo hilo la kilo 100 wanauza kwa Sh45,000 ikiwa ni pungufu zaidi ya mara mbili ya bei inayotumika Lindi. 

Bei hiyo inayotumika Mara ndiyo bei ya chini kabisa ikilinganishwa na maeneo mengine nchini.

Mahindi ni zao linalotegemewa na kaya nyingi nchini kwa chakula.

/
No matches found for this filter
26 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

Nukta TV

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

Nukta TV

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

Nukta TV