Tamasha kuwaunga mkono wapambanaji wa Corona kufanyika Aprili 18

April 7, 2020 2:04 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Litafanyika kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo Twitter, Instagramu na chaneli za televisheni.
  • Hadi sasa limekusanya zaidi ya Sh80 bilioni  kusaidia harakati za wadau wa afya kwenye kipindi cha mlipuko COVID-19.
  • Lady Gaga ataungana na wasanii wengine kibao wakiwemo John Legend na Burna Boy.

Dar es Salaam. Licha ya kusambaa kwa ugonjwa wa virusi vya Corona ambao umesababisha watu wasikusanyike pamoja, bado burudani ya muziki lazima iendelee.  

Shirika la Afya Duniani (WHO) likishirikiana na Shirika la Utetezi wa Kimataifa la Global Citizen limeandaa tamasha la muziki la  “Together At Home” yaani Pamoja Nyumbani linalolenga kuunga mkono juhudi za watumishi wa sekta ya afya wanaopambana na virusi vya corona.

“Tamasha hilo la mtandaoni litaonyesha umoja baina ya watu wote walioathirika na COVID-19 pamoja na kusherehekea na kuunga mkono mashujaa na watoa hudama za afya ulimwenguni wanaofanya kazi nzuri ya kuokoa maisha,” imesomeka taarifa ya Global Citizen.

Baadhi ya wadau watakaoonyesha tamasha la One worls: Together at home. Picha| The Verge.

Tamasha la “Together At Home “ ambalo mashirika hayo yameingia makubaliano na mwanamuziki wa miondoko ya muziki wa pop, Lady Gaga litaonyeshwa mubashara mtandaoni Aprili 18, 2020 kupitia mifumo mbalimbali ikiwemo Youtube na mtandao wa Instagram.

Mifumo mingine itakayoonyesha tamasha hilo ni pamoja na televisheni za MTV, Tidal, NBC, Alibaba na chaneli za M-Net. Pamoja na hayo, mitandao ya Twitter na Yahoo pia haijaachwa nyuma.


Zinazohusiana


Tamasha hilo ambalo hadi sasa limekusanya kitita cha Sh81 bilioni litahusisha wasanii wengine wakongwe wakiwemo Elton Johnn, Billie Eilish, Burna Boy, Johnn Legend na wengineo wengi wakiwemo Andrea Bocelli na Stevie Wonder.

Zaidi, watakaoendesha tamasha hilo ni pamoja na wachekeshaji  Jimmy Fallon, Jimmy Kimmel na Stephen Colbert.

Lady Gaga amesema, “Tunawashukuru wafanyakazi wote wa sekta ya afya nchini na duniani kote ambao wamekuwa mstari wa mbele kwenye kipindi cha COVID-19… mnachokifanya kinawaweka nyie wenyewe kwenye hatari kuisaidia dunia na tunawaheshimu.”

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Nukta TV

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Nukta TV

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Nukta TV