Bei ya viazi mviringo yaibua tofauti Mtwara, Rukwa

April 22, 2020 12:53 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Bei ya jumla inayotumika leo Mtwara ni zaidi ya mara mbili ya ile ya Rukwa. 
  • Gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya mkoani Mtwara linauzwa kwa Sh120,000, wakati masoko ya Rukwa  linauzwa kwa Sh45,000.

Dar es Salaam. Watumiaji wa viazi mviringo hasa kutengeneza chipsi katika Mkoa wa Mtwara leo watalala na maumivu kutokana na bei ya jumla ya zao hilo kuuzwa zaidi ya mara mbili ya bei inayotumika katika Mkoa wa Rukwa. 

Takwimu za mazao makuu ya chakula zilizotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara  leo (Aprili 22, 2020) zinaeleza kuwa gunia la kilo 100 la viazi mviringo katika masoko ya Mtwara linauzwa kwa Sh120,000, wakati masoko ya Rukwa linauzwa kwa Sh45,000.

Hiyo ina maana kuwa bei inayotumika leo Mtwara ni zaidi ya mara mbili  ya Rukwa, jambo linalowafaidisha zaidi wafanyabiashara ambao wamepeleka bidhaa hiyo mkoani humo. 

Bei hiyo inayotumika Mtwara ndiyo bei ya juu huku ya Njombe ikiwa ni ya chini ikilinganishwa na bei zinazotumika katika maeneo mengine nchini.

Viazi mviringo ni miongoni mwa mazao makuu ya chakula ambavyo vimekuwa vikutumiwa kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kukaanga chispi ambazo zinapendwa zaidi na mabachela. 

Enable Notifications OK No thanks